Maneno yake (Radhiya Allaahu ‘anhaa):
“… lakini alikuwa ni mwenye kuweza kujizuia vyema kuliko nyinyi.”
ni dalili kwamba ikiwa mwenye kufunga ataogopa kwa kumgusa mkewe kwamba matamanio yake yataamka au hatua za kuelekea tendo la ndoa, basi ni wajibu kwake kuacha busu na mguso kama kinga dhidi ya hilo, kwa sababu kuhifadhi swawm dhidi ya kuharibika ni wajibu na kila jambo ambalo wajibu halitimii isipokuwa kwa hilo, basi hilo pia ni wajibu.
Kigezo cha kufaa ni kwamba mwenye kufunga aweze kumiliki matamanio yake na kudhibiti nafsi yake. Ikiwa ataogopa kuingia katika jambo lililokatazwa, basi si halali kwake kumbusu wala kumgusa mkewe.
Ikiwa atambusu au kumgusa na akatokwa manii, basi swawm yake imeharibika. Ibn Qudaamah amesema:
”Tunajua hivo pasi na tofauti.”[1]
Hata hivyo ni jambo linahitaji kujadiliwa. Ibn Hazm ameona kwamba hawezi kufungua swawm kwa sababu ya busu au mguso hata kama atatokwa na manii na akatilia nguvu maoni hayo[2]. Imepokelewa kutoka kwa baadhi ya Maswahabah na wanafunzi wao ruhusa ya kumgusa mke kwa mwenye kufunga[3].
Kama akijichua mwenyewe na akatokwa na manii, basi swawm yake imeharibika kwa sababu hilo linafanana na busu katika kuamsha matamanio. Ibn Hazm ameona kuwa swawm yake haiharibiki, akitoa hoja kwamba hakuna dalili ya wazi ya kuvunjika swawm kwa hilo[4].
Na kama akimbusu au kumgusa na akatokwa madhiy, basi swawm yake haiharibiki kwa mujibu wa maoni zaidi ya wanazuoni. Madhiy ni maji yanayofanana na mkojo – na Allaah (Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.
[1] al-Mughniy (04/361).
[2] al-Muhallaa (06/205) na “Fath-ul-Baariy” (04/151).
[3] Muswannaf Ibn Abiy Shaybah (03/63).
[4] al-Muhallaa (06/205) na “al-Mughniy” (04/363).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/41)
- Imechapishwa: 12/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)