32. Matokeo ya kutoa fatwa kwa maoni binafsi

´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakika Allaah haondoi elimu baada ya kuwapa  nayo kwa kuinyakua moja kwa moja; bali huiondoa kwa kuwafisha wanazuoni pamoja na elimu yao. Hivyo hubakia watu wajinga wanaotoa fatwa kwa maono yao. Matokeo yake wakapotea na kuwapoteza wengine.”[1]

[1] al-Bukhaariy (7307) na Muslim (2673).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 36
  • Imechapishwa: 23/06/2025