32. Maneno ya al-Mughiyrah bin Shu´bah kuhusu mikono ya Allaah

33- ash-Sha´biy ameeleza kwamba amemsikia al-Mughiyrah bin Shu´bah akisema:

“Muusa alimuuliza Mola wake: “Ee Mola! Nikhabarishe nani ambaye ana manzilah ya juu zaidi Peponi?” Akasema: “Ni wale watu ambao karama zao Nimezipanda kwa mkono Wangu na nikaipigia muhuri; hakuna jicho imekwishaziona, sikio imekwishazisikia wala kupita moyoni mwa mtu.”[1]

Ameipokea Muslim.

[1] Muslim (312), at-Tirmidhiy (3198) na al-Bayhaqiy (690).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 28
  • Imechapishwa: 02/07/2019