Swali 32: Yepi maoni yenu juu ya kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa baada ya kumaliza kuswali? Je, kuna tofauti kati ya swalah ya faradhi na swalah iliyopendekezwa?
Jibu: Kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa imependekezwa na ni miongoni mwa sababu za kuitikiwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika Mola wenu ni Mwingi wa hayaa na Mkarimu. Anamuonea hayaa mja Wake anapomnyanyulia mikono Yake airudishe bure.”
Ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim kupitia kwa Salmaan al-Faarisiy.
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Allaah (Ta´ala) ni Mwema na anakubali kilicho chema tu. Allaah (Ta´ala) amewaamrisha yale aliyowaamrisha Mitume, akasema (Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ
“Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye pekee.”[1]
يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ
”Enyi Mitume! Kuleni katika vizuri na fanyeni mema, hakika Mimi kwa yale myatendayo ni Mjuzi.”[2]
Kisha akataja kuhusu mtu aliyesafiri safari ndefu, kachafuka na kajaa mavumbi na huku anayanyua mikono yake mbinguni akisema: “Ee Mola! Ee Mola! Wakati chakula chake cha haramu, kinywaji chake ni cha haramu, kivazi chake ni cha haramu na anashibishwa na haramu. Vipi basi atajibiwa?”
Ameipokea Muslim.
Hata hivyo mikono haikusuniwa katika yale maeneo yaliyokuwepo wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hakunyanyua ndani yake. Baadhi ya maeneo hayo ni kama baada ya kumaliza zile swalah tano, kati ya Sujuud mbili, kabla ya kutoa Tasliym kutoka ndani ya swalah na wakati wa Khutbah ya ijumaa na Khutbah ya ´iyd mbili. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakunyanyua mikono katika maeneo haya. Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye kiigizo chema katika yale anayoleta na kuacha. Lakini anapoomba kuteremshiwa mvua katika Khutbah ya ijumaa au Khutbah ya ´iyd mbili itasuniwa kunyanyua mikono. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kuhusu swalah iliyopendekezwa sijui kizuizi cha kukataza kunyanyua mikono baada yake wakati wa kuomba du´aa kwa ajili ya kutendea kazi ueneaji wa dalili. Lakini ni kutodumu juu ya jambo hilo. Kwa sababu mambo hayo hayakuthibiti kufanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Angeyafanya baada ya kila swalah iliyopendekezwa basi yangenakiliwa kutoka kwake. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anh) wamenukuu maneno na matendo yake katika hali zake za safari, hali zake za ukazi na hali zake nyinginezo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na (Radhiya Allaahu ´anhum).
Kuhusu Hadiyth inayotambulika eti Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Swalah ni kule kujivunjavunja, kunyenyekea na unyanyue mikono yake kwa kusema: “Ee Mola! Ee Mola!”
ni dhaifu. Hayo yamesemwa wazi na Haafidhw Ibn Hajar na wengineo.
[1] 02:172
[2] 23:51
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 35-36
- Imechapishwa: 23/08/2022

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 35-36
Imechapishwa: 23/08/2022
https://firqatunnajia.com/32-kigezo-cha-unyanyuaji-mikono-wakati-wa-kuomba-duaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)