32. Haifai kabisa kumkufurisha mtu kwa dhati yake?

Swali 32: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema:

“Hakuna kabisa hukumu ya kumkufurisha mtu binafsi kwa dhati yake”?

Jibu: Maneno haya si sahihi. Mtu binafsi kwa dhati yake anakufurishwa. Sisi tunamkufurisha myahudi kwa dhati yake, mnaswara kwa dhati yake na yule ambaye hoja imesimama dhidi yake anakufuru kwa dhati yake. Maana ya maneno haya – kutomkufurisha mtu yeye kama yeye – ni kwamba hapatakuwa na kafiri yeyote kabisa. Lakini yule ambaye hoja imesimama dhidi yake miongoni mwa wale wanaofanya kufuru, aidha mnaswara, myahudi na wenye kuabudia masanamu na mizimu, wanakufurishwa. Ambaye ana utata basi unapaswa kuondolewa.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 70
  • Imechapishwa: 09/01/2026