Swali 31: Una nasaha gani mnayoitoa kwa wanafunzi wanaotaka kuelewa vizuri masuala ya Tawhiyd na shirki, pamoja na masuala ya imani na ukafiri? Na ni vitabu gani vilivyozungumzia masuala haya kwa kina?
Jibu: Nasaha yangu kwa wanafunzi ni kujitahidi kutafuta elimu, kuwa na juhudi katika hilo, kuhudhuria duara za elimu, darsa na mihadhara ya wanazuoni na kusoma vitabu vyenye manufaa kama vile vitabu vya Imamu Muhammad bin ´Abd-il-Wahhaab, maimamu wa ulinganizi, vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah pamoja na ‘Allaamah Ibn-ul-Qayyim. Shaykh Muhammad bin ´Abd-il-Wahhaab ameandika kitabu muhimu kuhusu ukafiri wa mwenye kuacha Tawhiyd kiitwacho ”Mufiyd-ul-Mustafiyd fiy Kufr Taarik-il-Tawhiyd”. Pia kuna kitabu ”al-Kalimaaat-ul-Naafi’ah fiy al-Mukaffiraat al-Waaqi’ah” kilichoandikwa na ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Abd-il-Wahhaab. Ibn-ul-Qayyim ana vitabu vingi kuhusu masuala haya. Shaykh-ul-Islam Ibn Taymiyyah amebainisha sana masuala haya katika vitabu vyake vya fatwa. Aidha wanazuoni wa kila madhehebu – kama vile Hanaabilah, Shaafi´iyyah, Maalikiyyah na Ahnaaf – wanaweka mlango maalum katika vitabu vya Fiqh kwa jina ”Mlango wa hukumu ya mwenye kuritadi” unaozungumzia hukumu ya yule anayekufuru baada ya Uislamu. Wanabainisha aina mbalimbali za ukafiri, ikiwemo ukafiri wa maneno, vitendo na kiitikadi. Kwa hivyo ni muhimu kurejea kwenye vitabu hivi.
Miongoni mwa madhehebu, Ahnaaf wameandika sana katika mlango wa hukumu ya murtadi na wameainisha aina nyingi za ukafiri zinazoweza kufikia makundi mia nne. Wameeleza pia kwamba miongoni mwa aina za ukafiri ni, kwa mfano, kudharau msikiti au msahafu kwa kutumia maneno kama “kijimsikiti kidogo” au “kijimsahafu kidogo” kwa mtindo wa dharau. Kwa hiyo tunawataka wanafunzi wapatilize mambo haya. Kitabu ”ad-Durar as-Saniyyah fiyl-Ajwibah an-Najdiyyah” kina juzuu nzima inayozungumzia ukafiri na aina zake. Vyanzo na marejeo kwa masuala haya vinapatikana kwa wingi na himdi zote ni stahiki ya Allaah.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 67-69
- Imechapishwa: 09/01/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 67-69
Imechapishwa: 09/01/2026
https://firqatunnajia.com/31-nasaha-kwa-wanafunzi-kufanya-bidii-katika-kujifunza-elimu-na-baadhi-ya-vitabu-muhimu-vya-aqiydah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket