Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Na Allaah ametuneemesha kwa Kitabu Chake ambacho:
تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ
“Kinachobainisha kila kitu na ni mwongozo na rehema na bishara kwa waislamu.” (16:89)
MAELEZO
Allaah ametuneemesha kwa Kitabu Chake kitukufu ambacho:
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ
“Haitokifikia ubatili mbele yake na wala nyuma yake; ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima ya kila kitu, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.” (41:42)
Amekifanya (Subhaanahu wa Ta´ala) kuwa ni kielelezo chenye kubainisha kila kitu ambacho mwanaadamu anakihitajia katika maisha haya na Aakhirah. Ubainifu wa Qur-aan kuyabainisha mambo kumegawanyika sehemu mbili:
2 – Inabainisha jambo maalum. Mfano wa hilo ni maneno Yake (Tabaarak wa Ta´ala):
حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ
“Mmeharamishiwa nyamafu na damu na nyama ya nguruwe.” (05:03)
Vilevile amesema (Ta´ala):
حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ
“Mmeharamishiwa [kuwaoa] mama zenu, na mabinti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na makhalati zenu, na mabinti wa kaka, na mabinti wa dada, na mama zenu ambao wamekunyonyesheni, na ndugu zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu ambao mmewaingilia – lakini ikiwa hamkuwaingilia basi hakuna dhambi [kuwaoa] – na [mmeharamishwa] wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu na kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika Allaah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. Na [Mmeharamishiwa pia] wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume – ni Shari’ah ya Allaah kwenu. Na mmehalalishiwa [wengineo] wasiokuwa hao.” (04:23-24)
2 – Ubainifu uwe kwa njia ya kuashiria kitu kilichobainishwa. Mfano wa hilo ni maneno Yake (Ta´ala):
وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ
“Na Allaah amekuteremshia Kitabu na Hekima.” (04:113)
Hapa Allaah (Ta´ala) ameashiria hekima, ambayo ni Sunnah. Sunnah inaibainisha Qur-aan. Mfano mwingine ni maneno Yake (Ta´ala):
فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
“Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa hamjui.” (16:43)

“Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa hamjui.” (21:07)
Hili linabainisha kuwa sisi tunatakiwa daima kurejea kwa wale waliotakhasusi juu ya jambo fulani. Kuna mwanachuoni aliyesimulia kuwa kuna mnaswara aliyemjia ili kuitukana Qur-aan Tukufu. Mnaswara huyo alikuwa amekaa kwenye mgahawa akamwambia:
“Ubainifu uko wapi wa namna ya kupika chakula hiki?” Mtu yule akamwita mmiliki wa mgahawa na akamwambia: “Twambie ni vipi unapika chakula hichi?” Yule mmiliki wa mgahawa akawaeleza. Yule mwanachuoni akasema: “Namna hii imetajwa katika Qur-aan.” Yule mnaswara akastaajabu na kusema: “Vipi?” Yule mtu akasema: “Allaah (´Azza wa Jall) anasema:

Ametubainishia ufunguo wa elimu wa mambo kwa kuwauliza wale watambuzi wa mambo hayo. Hili ni katika ubainifu wa Qur-aan bila ya shaka. Kwa njia hiyo inazingatiwa kuwa ni ufunguo wa elimu kurejea kwa wale wajuzi.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 53
- Imechapishwa: 04/11/2023

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 53
Imechapishwa: 04/11/2023
https://firqatunnajia.com/31-mlango-wa-06-qur-aan-inabainisha-kila-kitu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)