Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

27- Amewakadiria makadirio yao.

MAELEZO

Allaah (Jalla wa ´Alaa) amekadiria makadirio yote. Hakuumba viumbe hivi pasi na makadirio:

وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَائِنُهُ وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلَّا بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ

“Hakuna kitu chochote isipokuwa Tuna hazina zake na hatukiteremshi isipokuwa kwa kiwango maalum.”[1]

Kila kitu kimekadiriwa na Allaah. Sifa hazibadiliki wala hazigeuki. Allaah amekadiria mwili wa mtu, hisia zake, viungo vyake, uundwajii wake na uzani wake mpaka akaweza kuwa mtu mwenye kuweza kutembea na kusimama. Lau kiungo kimoja wapo kitapatwa na ulemavu basi mwili mzima unakuwa na kasoro. Kadhalika inahusiana na viumbe wengine wote:

اللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَحْمِلُ كُلُّ أُنثَىٰ وَمَا تَغِيضُ الْأَرْحَامُ وَمَا تَزْدَادُ ۖ وَكُلُّ شَيْءٍ عِندَهُ بِمِقْدَارٍ

“Allaah anajua abebacho mimba ya kila mwanamke na kinachopunguza matumbo ya uzazi na kinachozidisha na kila kitu Kwake ni kwa kipimo.”[2]

Kila kitu kina makadirio yake na kimepangiliwa na makadirio ya kila mmoja ni yenye kutofautiana na ya mwengine.

[1] 15:21

[2] 13:08

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 48
  • Imechapishwa: 24/09/2019