169 – Ibraahiym bin Hajjaaj as-Saamiy ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa ´Aliy bin Zayd, kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab… kutoka kwa Humayd pia, kutoka kwa Muwarriq, ambaye ameeleza:

“Sa’d bin Maalik na ‘Abdullaah bin Mas’ud walimtembelea Salmaan ambapo akalia. Wakasema: ”Kipi kinachokuliza, ee Abu ´Abdillaah?” Akasema: “Kutokana na ahadi tuliyompa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  na hakuna yeyote katika sisi ambaye ameihifadhi: ”Mmoja wenu anufaike na ulimwengu huu kama maandalizi ya mpanda farasi.”[1]

170 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ibn ´Uyaynah ametukhabarisha, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Yahyaa bin Ja´dah, kutoka kwa Khabbaab, ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika hapana vyenginevyo inamtosha mmoja katika dunia sawa na maandalizi ya mpanda farasi.”[2]

171 – Hudbah ametukhaabirisha: Hammaad bin Salamah ametukhaabirisha, kutoka kwa Sa´iyd al-Jariyriy, kutoka kwa Abu Nadhwrah, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mawlah, kutoka kwa Buraydah, ambaye amesimulia kuwa  Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Inamtosha mmoja wenu katika dunia kuwa na mfanya kazi na makazi.”[3]

[1] at-Twabaraaniy (6160).

[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (3317).

[3] Ahmad (22534). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (5464).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 42
  • Imechapishwa: 20/07/2025