29. Kitendo cha kidini kwa ajili ya kuitafuta dunia

168 – Ibraahiym bin al-Hajjaaj as-Saamiy ametukhabarisha: ´Abdul-´Aziyz bin Muslim ametukhabarisha, kutoka kwa ar-Rabiy´ bin Anas, kutoka kwa Abul-´Aaliyah, kutoka kwa Ubayy bin Ka´b, ambaye amesimulia kuwa  Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wape bishara njema ummah huu ya utukufu, enzi na kumakinishwa. Atakayefanya miongoni mwao kitendo cha Aakhirah kwa ajili ya dunia yake, basi huko Aakhirah hatopata fungu lolote.”[1]

[1] Ahmad (20716). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (2825).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 41
  • Imechapishwa: 07/07/2025