Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nimekuacheni katika njia nyeupe kabisa; usiku wake ni kama usiku wake. Hatopotea nayo baada yangu isipokuwa mwangamivu.”[1]

“Allaah hakutuma Mtume yeyote isipokuwa ilikuwa ni wajibu kwake kuwaelekeza Ummah wake katika yale yenye kheri anayoyajua kwao na kuwakataza yale yenye shari anayoyajua kwao.”[2]

MAELEZO

Mwishoni mwishoni wakati wa kufa kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Nimekuacheni katika njia nyeupe kabisa; usiku wake ni kama usiku wake. Hatopotea nayo baada yangu isipokuwa mwangamivu.”

Bi maana njia ya wazi na safi, nayo ni Sunnah zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Hatopotea nayo baada yangu isipokuwa mwangamivu.”

Atakayeshika njia yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atafika kwa Allaah na kusalimika kutokana na maangamivu, na yule atakayeiacha ataangamia, kwa sababu ameshika njia isiyo.

[1] Ahmad (4/126), Ibn Maajah (43) na al-Haakim (1/95).

[2] Muslim (1844).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 31/07/2024