Swali 90: Ni ipi hukumu ya kumuasi na kwenda kinyume na watawala katika yasiyokuwa haramu wala maasi?
Jibu: Jambo hilo ni haramu kali, kwa sababu ni kumuasi Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1]. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ
“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yule mwenye kumtii kiongozi basi amenitii mimi, na yule mwenye kumuasi kiongozi ameniasi mimi.”[3]
Kumuasi mtawala kunasababisha mgawanyiko, ummah kutofautiana, kuzuka kwa fitina na ukosefu wa amani. Kiapo cha usikivu kwa mtawala kinapelekea kumtii katika mema, kujivua katika utiifu wake kunazingatiwa ni khiyana. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَأَوْفُواْ بِعَهْدِ اللّهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ وَلاَ تَنقُضُواْ الأَيْمَانَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ اللّهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلاً إِنَّ اللّهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ
“Timizeni ahadi ya Allaah mnapoahidi na wala msivunje viapo baada ya kuvifunga na mmekwishamfanya Allaah kuwa ni mdhamini wenu; hakika Allaah anajua yale mnayoyafanya.”[4]
Kuvunja ahadi ni miongoni mwa sifa za wanafiki.
[1] Imaam Ismaa´iyl bin Yahyaa al-Muzaniy amesema katika kitabu chake ”Sharh-us-Sunnkwaah”kwenda Tripoli, Afrika Kaskazini:
”Mtawala anatakiwa kutiiwa katika yale yenye kumridhisha Allaah na si katika yale yenye kumkasirisha Allaah.”
Pengine mtu akaona kuwa hatuwezi kumnyamazia mtawala wakati anapodhulumu na kukandamiza. Jibu letu juu ya hilo ni kurejesha tofauti na mizozo yetu katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Ta´ala):
فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا
”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”
Kwa msemo mwingine Allaah ametuamrisha kumtii mtawala katika yasiyokuwa maasi. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.” (4:59)

”Msikilize na umtii kiongozi hata kama atakupiga mgongo wako na kuchukua mali yako.” (Tazama ”Fath-ul-Baariy” (8/13))
Ibn Abiyl-´Izz al-Hanafiy (Rahimahu Allaah) amesema:
”Kuhusu kumtii mtawala hata kama ni mwenye kufanya dhuluma, ni kwa sababu kufanya uasi dhidi yao kunapelekea madhara makubwa kuliko ile dhuluma yao. Bali kule kusubiri juu ya dhuluma yao kunafuta madhambi na kunaongeza thawabu. Allaah (Ta´ala) hakuwasalitisha juu yetu isipokuwa ni kwa sababu ya matendo yetu, kwa sababu mtu anavuna kile alichopanda. Kwa ajili hiyo tunatakiwa kuhakikisha tunaomba msamaha kwa wingi, kutubu na kuyatengeneza matendo.” (Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 381)
[2] 4:59
[3] Ibn Abiy ´Aaswim (1065-1068). Swahiyh.
[4] 16:91
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 221-222

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 221-222
https://firqatunnajia.com/90-ni-ipi-hukumu-ya-kuwaasi-watawala/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)