Swali 91: Ni ipi hukumu ya kusababisha mpasuko kati ya watawala na wananchi, kufungua kamati na kuanzisha miradi bila idhini yao?

Jibu: Haijuzu kwa mwananchi yeyote kuanzisha kamati au miradi inayosimamia chochote katika mambo ya ummah isipokuwa kwa idhini ya mtawala. Kwa sababu kufanya hivo kunazingatiwa ni kujitoa katika utiifu wao na ukiukaji usiofaa na pia hilo linasababisha vurugu na kupotea kwa wajibu katika jamii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 222-223
  • Imechapishwa: 31/07/2024