Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:
“Inatakiwa kuamini kuwa Allaah atawazungumzisha waja siku ya Qiyaamah, hakuna baina yao na baina Yake mkalimani. Hili linatakiwa kuaminiwa na kusadikishwa.”
MAELEZO
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa Mola Wake atamzungumzisha bila ya kuwepo baina yake na baina Yake mkalimani.”[1]
Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ataita siku ya Qiyaamah:
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ أَيْنَ شُرَكَائِي قَالُوا آذَنَّاكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٍ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَدْعُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَظَنُّوا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ
“Siku Atakayowaita: “Wako wapi [sasa hao] washirika Wangu?” – watasema wakijibu: “Tunakiri Kwako hapana miongoni mwetu anayeshudia [kwamba wapo].” Yatawapotea yale waliyokuwa wakiyaomba kabla na watayakinisha hawana mahali pa kukimbilia.”[2]
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ
“Siku Atakayowaita na aseme: “Wako wapi hao washirika Wangu mliokuwa mkinishirikisha nao?”[3]
Wito hauwi isipokuwa kwa herufi na sauti. Wito ni maneno. Atanadi kwa watu wa Peponi:
“Mmeridhika? Niwapeni zaidi?”[4]
Atazungumza na kuongea. Atamzungumzisha (Subhaanahu wa Ta´ala) mmoja baada ya mwingine pasi na mkalimani. Atawazungumzisha watu wote. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) siku zote anasifika na ukamilifu huu. Hii ni miongoni mwa sifa Zake (Tabaarak wa Ta´ala) kamilifu ya kwamba anazungumza na watu siku ya Qiyaamah kama Alivyozungumza na Muusa, Muhammad, Jibriyl na Malaika (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Makusudio ni kwamba Atazungumza na waumini siku ya Qiyaamah.
[1] al-Bukhaariy (6539) na Muslim (1016).
[2] 41:47-48
[3] 28:62
[4] Muslim (181).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 392
- Imechapishwa: 26/08/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 392
Imechapishwa: 26/08/2017
https://firqatunnajia.com/30-kuzungumza-kwa-allaah-na-waumini-siku-ya-qiyaamah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)