Shaykh Bakr amesema pindi alipokuwa akianza makosa yake:

“1- Nimetazama ukurasa wa kwanza wa yaliyomo na kuona kuwa kichwa cha khabari kimekusanya misingi ya ukafiri, ukanamungu na uzandiki kwa Sayyid Qutwub. Ukiongezea nadharia ya kwamba viumbe vyote ni Allaah, Qur-aan imeumbwa, kwamba inajuzu kwa asiyekuwa Allaah kuweka Shari´ah, upindukaji mipaka katika kukanusha sifa za Allaah (Ta´ala), ya kwamba hakubali Hadiyth zilizopokelewa kwa mapokezi mengi (Mutawaatir), anatilia shaka mambo ya ´Aqiydah ambayo ni wajibu kuyayakinisha na kadhalika. Haya yanafanya ngozi ya muumini kusisimka. Nasikitika kuona wanachuoni wa waislamu wa ulimwengu hawakuona makosa haya yenye kuangamiza. Ni vipi mtu anaweza kuoanisha hili na vitabu vya Sayyid Qutwub kuenea ulimwengu mzima? Watu wote wanapata faida kwayo hata na wewe katika baadhi ya vitabu vyako. Hivyo nikaanza kulinganisha kati ya kichwa cha khabari na mada na kuona kuwa haviendani. Kwa ujumla inahusiana na vichwa vya khabari vya kushtua ambavyo vinamfanya msomaji kumtukana Sayyid Qutwub (Rahimahu Allaah). Kuhusiana na msomaji aliye angalau na uelewa mdogo, atakuta athari ya kinyume pindi ataposoma maudhui ndani ya kitabu na kwa ajili hiyo anarudi kuwa na mapenzi kwa vitabu vya Sayyid Qutwub (Rahimahu Allaah). Sipendelei mimi na waislamu wengine wote kutumbukia kwenye madhambi. Hakika ni katika dhuluma mbaya kwa mtu kuyatoa matendo yake mema kumpa mtu ambaye ana chuki na uadui kwake.”

Mosi: Ni lipi kosa la Rabiy´ ikiwa Sayyid Qutwub amejichagulia mfumo huu peke yake na akaandika makosa haya ya kuangamiza kwenye vitabu vyake ambayo yameenea ulimwenguni kote? Ikiwa Rabiy´ ameyaona makosa haya ya kuangamiza na khatari yake halafu akawafikishwa na Allaah kuyakemea kwa dalili na hoja kutoka katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maneno ya Salaf, analaumika kwa wenye busara kusimamia jambo la wajibu hili ambalo ni lazima litekelezwe na baadhi ya waislamu au anatakiwa kushukuriwa na kunusuriwa? Haya yanaenda sambamba na maamrisho ya Allaah juu ya kusaidiana katika wema na uchaji Allaah na maamrisho ya Allaah na Mtume Wake juu ya kuinusuru dini hii tukufu na waislamu.

Pili: Shaykh Bakr amesema wazi kuwa ameyakuta makosa haya yenye kuangamiza katika yaliyomo kwenye kitabu. Katika yaliyomo kwenye kitabu na ndani ya kitabu mna vilevile:

1- Adabu ya Sayyid Qutwub na Mtume wa Allaah Muusa.

2- Msimamo wa Sayyid Qutwub kwa ´Uthmaan na kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kabla ya kuanza kukiandika kitabu nilimweleza kuhusu matusi ya Sayyid kwa ´Uthmaan na kwa Maswahabah katika “al-´Adalah al-Ijtimaa´iyyah”. Nikamuuliza kuhusu kichwa cha khabari cha kitabu kilicho na nguvu na uwazi. Ni kwa nini alipuuza vichwa vya khabari hivi viwili? Ni kwa nini alipuuza matusi ya Sayyid kwa Nabii mtukufu na Mtume aliyesemezwa na Allaah?

Ni kwa nini alipuuza matusi ya Sayyid Qutwub kwa khaliyfah wa tatu mwongofu ´Uthmaan bin ´Affaan na ndugu zake katika Maswahabah?

Ni kwa nini ´Aqiydah yake haikutikisika kama kuwapenda na kuwaheshimu Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ule uwajibu wa kuwatetea? Angalau kwa uchache angelimnusuru yule mwenye kutetea heshima zao tukufu.

Tatu: Shaykh Bakr amenikosoa ikiwa ni pamoja na kwamba nimesema kuwa Sayyid Qutwub hakubali Hadiyth zilizopokelewa kwa njia tele. Hivyo nataka kusema mambo mawili:

1- Msimamo wa Sayyid Qutwub juu ya Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maneno ya Mitume na kwamba ni fikira za kiuanaadamu.

Mlango wa kumi na nne wa kitabu “Adhwaa´ Islaamiyyah ´alaa ´Aqiydati Sayyid Qutwub wa Fikrih” nimeupa jina “Sayyid Qutwub hakubali maelezo yaliyopokelewa kwa wapokezi wachache na wala hakubali Hadiyth zilizopokelewa kwa mapokezi mengi”. Baada ya hapo chini ya kichwa cha khabari hichi nikataja maneno ya Sayyid Qutwub alipokuwa akifasiri Suurah “al-Falaq”:

“Kumepokelewa baadhi ya mapokezi na baadhi yake ni sahihi, lakini hayakupokelewa na wapokezi wengi… ´Aqiydah haichukuliwi kutoka katika Hadiyth zilizopokelewa kwa wapokezi wachache. Marejeleo ni Qur-aan. Ili zichukuliwe Hadiyth katika msingi wa ´Aqiydah, imeshurutishwa iwe imepokelewa na wapokezi wengi.”[1]

Shaykh Bakr ameyakemea haya kwa njia ya ajabu na hakumkemea Sayyid Qutwub kwa kanuni hii ya khatari inayotupilia mbali Hadiyth nyingi Swahiyh katika ´Aqiydah. Nimesema vilevile kuwa hatumii hoja hata kwa Hadiyth zilizipokelewa na wapokezi wengi katika milango ya ´Aqiydah. Mfano wa Hadiyth hizo ni kulingana kwa Allaah juu ya ´Arshi, kuja kwa Allaah, waumini kumuona Allaah siku ya Qiyaamah na kushuka kwa ´Iysaa. Bali anafikia hata kuzipotosha Aayah za Qur-aan zinazohusiana na I´tiqaad hizi. Ametakasika Allaah, Mola wa ´Arshi kubwa. Ninauliza ni msimamo upi Shaykh Bakr atachukua pindi atapoona kuwa mtazamo wa Sayyid juu ya Sunnah ya Mtume na maneno ya Mitume – kukiwemo Mtume wa Allaah Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – ya kwamba ni fikira za kiuanaadamu. Soma yaliyoandikwa na Sayyid Qutwub:

“Chanzo hichi cha kiungu kimetujia kwa mtazamo huu – nayo ni Qur-aan tukufu – unabainisha kuwa ni zawadi kutoka kwa Allaah na rehema kutoka kwa Allaah kwenda kwa wanaadamu na kwamba ni fikira za kiuanaadamu – tukianzia kwa fikira za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na fikira za Mitume wengine wote kwa kuzingatia kuwa wote wametumwa kwa mtazamo huu – hauna vyanzo sawa. Aliuchukua ili aongoke yeye na kuongoza. Uongofu huu ni zawadi kutoka kwa Allaah na kwa ajili hiyo unakubaliwa na wengine. Kazi ya Mtume – pasi na kujali ni Mtume gani – juu ya mtazamo huu ni kufikisha kwa umakini na uaminifu pasi na kuchanga Wahy na fikira yoyote ile ya kiuanaadamu, au kama jinsi Allaah anavyoita “wahy”.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakukataza Sunnah isiandikwe eti kwa sababu ni fikira za kiuanaadamu, isipokuwa ni kwa malengo mengine yanayojulikana na wanachuoni wenye kushikamana na Sunnah na uongofu. Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zimetakasika na mtazamo alionao Sayyid Qutwub. Sayyid Qutwub anasema [kuhusu Qur-aan]:

“Dhamana hii juu ya chanzo cha mtazamo huu ndio unaoipa hadhi ya msingi wake na hadhi ya ukubwa wake. Mtazamo huu pekee ndio wenye kuaminika kwa kuwa ndio ambao mtu anajua kuwa umekingwa na mapungufu, ujinga na matamanio. Sifa hizi zinapatikana katika matendo ya wanaadamu wote, ambayo tunaweza kuyaona katika mitazamo ya wanaadamu wote kutoka kwa waabudu mizimu na wanafalsafa, ´Aqiydah za kimbingu za kale ambazo wanaadamu wamejichanganya ndani yake.”[3]

Hakumvua bwana wa Manabii na Mitume na wala hakuvua Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokamana na kasoro hizi.

Ni kweli kuwa Qur-aan na vitabu vilivyoteremshwa viko namna hiyo bali zaidi ya hivyo, lakini Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zilizothibiti pia ni chanzo chenye kuaminika kwa waumini. Vilevile imetakasika kutokamana na kasoro, ujinga na matamanio. Hali kadhalika maneno ya Mitume wengine wote (´alayhim-us-Swalaatu was-Salaam).

Huku ni kuangusha kwa kukusudia uaminifu wa Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio nadharia walionayo Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal, katika Jahmiyyah, Mu´tazilah na Qur-aaniyyah, juu ya Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo Allaah amesema juu yake:

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ

“Wala hatamki kwa matamanio yake. Hayo ayasemayo si chochote isipokuwa ni Wahy anaofunuliwa.[4]

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ

“Tumekuteremshia Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao na huenda wakapata kutafakari.”[5]

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Basi naapa kwa Mola wako hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha.”[6]

Sayyid Qutwub amesema katika “al-Muqawwamaat”:

“Baada ya masomo marefu tunaitakidi kuwa Qur-aan inatosheleza kubainisha uhalisia ambao mtazamo wa Kiislamu umejengwa juu yake. Hakuna kingine kilichoko nje kinachohitajika katika ubainifu huu. Wakati wa utafiti ni lazima kwa msomaji kuirejelea peke yake aone kuwa kuna ubainifu wa kila kitu.”[7]

Iko wapi Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Ni kwa nini unaonelea kuwa mtu arejee katika Qur-aan peke yake na kufuta Sunnah? Qur-aan na Sunnah vyote viwili ni misingi, hoja na dalili kutoka kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala), Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa maimamu wa Uislamu wanaojulikana. Wewe ni nani mpaka uje na mfumo huu unaoenda kinyume na mfumo wa Allaah, Mtume Wake na maimamu wa Uislamu?

[1] الفلق”> http://www.daawa-info.net/NewThelal.php?versnumber=5&suraname=113&nameofsora=الفلق

[2] Khaswaa-is-ut-Taswawwur al-Islaamiy wa Muqawwimaatuh, uk. 50.

[3] Khaswaa-is-ut-Taswawwur al-Islaamiy wa Muqawwimaatuh, uk. 51.

[4] 53:03-04

[5] 16:44

[6] 04:65

[7] Uk. 86