Inampasa awahi mapema kusoma kwa mwalimu mwanzoni mwa mchana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ee Allaah! Bariki ummah wangu katika mapema yao!”[1]
Inampasa kudumisha kusoma alichohifadhi na haifai kumpa mwingine zamu yake, kwani kupeana kipaumbele katika mambo ya ´ibaadah kunachukizwa, tofauti na kupeana katika mambo ya nafsi ambako kunapendekezwa. Ikiwa mwalimu ataona manufaa katika kutoa nafasi kwa mwingine katika baadhi ya nyakati kwa maana ya Kishari´ah na akamwelekeza hivyo, basi atekeleze amri yake.
Miongoni mwa mambo yanayomlazimu na kusisitizwa kwake ni kwamba asimhusudu yeyote miongoni mwa wenzake au wengineo kwa fadhilah aliyompa Allaah. Asijivunie nafsi yake kwa kile alichompa Allaah. Tumeshatangulia kufafanua hilo katika adabu za mwalimu.
Njia ya kuondoa majivuno ni kwamba ajikumbushe nafsi yake kuwa hakupata alichopata kwa uwezo wala nguvu zake – bali hiyo ni fadhilah kutoka kwa Allaah (Ta´ala). Haifai ajivunie kitu ambacho hakukibuni, bali Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye amekiweka ndani yake.
Njia ya kuondoa husuda ni kujua kwamba hekima ya Allaah (Ta´ala) imekusudia kuweka fadhilah hii kwa huyu. Hivyo inampasa asipinge hilo na wala asichukie hekima ambayo Allaah (Ta´ala) ameitaka na wala hakuichukia – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] Abu Daawuud (2606), at-Tirmidhiy (1212) na Ibn Maajah (2236). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (1212).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 37
- Imechapishwa: 26/08/2026
Inampasa awahi mapema kusoma kwa mwalimu mwanzoni mwa mchana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ee Allaah! Bariki ummah wangu katika mapema yao!”[1]
Inampasa kudumisha kusoma alichohifadhi na haifai kumpa mwingine zamu yake, kwani kupeana kipaumbele katika mambo ya ´ibaadah kunachukizwa, tofauti na kupeana katika mambo ya nafsi ambako kunapendekezwa. Ikiwa mwalimu ataona manufaa katika kutoa nafasi kwa mwingine katika baadhi ya nyakati kwa maana ya Kishari´ah na akamwelekeza hivyo, basi atekeleze amri yake.
Miongoni mwa mambo yanayomlazimu na kusisitizwa kwake ni kwamba asimhusudu yeyote miongoni mwa wenzake au wengineo kwa fadhilah aliyompa Allaah. Asijivunie nafsi yake kwa kile alichompa Allaah. Tumeshatangulia kufafanua hilo katika adabu za mwalimu.
Njia ya kuondoa majivuno ni kwamba ajikumbushe nafsi yake kuwa hakupata alichopata kwa uwezo wala nguvu zake – bali hiyo ni fadhilah kutoka kwa Allaah (Ta´ala). Haifai ajivunie kitu ambacho hakukibuni, bali Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye amekiweka ndani yake.
Njia ya kuondoa husuda ni kujua kwamba hekima ya Allaah (Ta´ala) imekusudia kuweka fadhilah hii kwa huyu. Hivyo inampasa asipinge hilo na wala asichukie hekima ambayo Allaah (Ta´ala) ameitaka na wala hakuichukia – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] Abu Daawuud (2606), at-Tirmidhiy (1212) na Ibn Maajah (2236). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (1212).
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 37
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/29-unyenyekevu-wa-mwanafunzi/