Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Sharti ya sita ni kufunika viungo ambavyo havitakiwi kuonekana (´Awrah). Wanachuoni wote wameafikiana juu ya kuharibika kwa swalah ya mwenye kuswali uchi ilihali anaweza kujifunika. Mpaka wa uchi wa mwanaume ni kuanzia kwenye kitovu mpaka kwenye magoti na vivyo hivyo kuhusu mjakazi. Ama mwanamke aliyehuru, mwili wake wote huzingatiwa kuwa ni haramu kuuonesha isipokuwa uso. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):
يَا بَنِي آدَمَ خُذُواْ زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ
“Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu [mnapoenda] katika kila msikiti.”[1]
Bi maana katika kila swalah.
MAELEZO
Wanazuoni wote wameafikiana juu ya kuharibika swalah ya aliyeswali akiwa uchi hali ya kuwa ana uwezo wa kujisitiri.
Kikomo cha uchi inapokuja kwa mwanaume ni kuanzia kwenye kitovu hadi kwenye goti. Vivyo hivyo kuhusu mjakazi. Ama mwanamke huru mwili wake wote ni uchi isipokuwa tu uso wake. Dalili ya hilo ni maneo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

“Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu [mnapoenda] katika kila msikiti.”
Kwa maana wakati wa kila swalah.
Katika hali ya dhiki ni lazima kufunika uchi kwa ujumla katika swalah na hata nje ya swalah kwa kile kisichouchora mwili, isipokuwa kwa mke na yule anayemilikiwa na mkono wa kuume. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Funika ucho wako isipokuwa mbele ya mke wako au yule aliye chini ya milki ya mkono wako.”
Ameipokea at-Tirmidhiy (2769) na wengineo kupitia kwa Mu´aawiyah bin Haydah. at-Tirmidhiy amesema: ”Hadiyth hii ni nzuri.” Tazama ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (1810).
[1] 07:31
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 30-31
- Imechapishwa: 26/05/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 30-31
Imechapishwa: 26/05/2026
https://firqatunnajia.com/29-sharti-ya-sita-ya-swalah-ni-kufunika-viungo-visivyotakiwa-kuonekana/