Kikomo cha uchi inapokuja kwa mwanaume ni kile kilicho juu ya goti mpaka chini ya kitovu. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Iwapo mmoja wenu atamuozesha mtumishi wake, mjakazi wake au mfanyakazi wake, basi asitazame yale yaliyo chini ya kitovu na juu ya goti.”

Ameipokea Abu Daawuud (496) kupitia kwa ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na cheni ya wapokezi ni nzuri.

Maana yake ni kwamba bwana akimuozesha mtumishi wake, ambaye ni mjakazi wake, basi si halali kwa huyo mtumishi kutazama uchi wa bwana wake, kwa sababu kwa kumuozesha mjakazi manufaa ya kustarehe naye yanahama kutoka kwake kwenda kwa mume wake. Hivyo hutoka katika hukumu ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Funika ucho wako isipokuwa mbele ya  mke wako au yule aliye chini ya milki ya mkono wako.”

Kinachojulisha vilevile ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Funika paja lako, kwani hakika ni sehemu ya uchi.”

Ameipokea at-Tirmidhiy (2798) kupiita kwa Jarhad. at-Tirmidhiy ameema: ”Hadiyth hii ni nzuri.”

al-Bukhaariy amesema katika ”as-Swahiyh” yake:

”Mlango yanayotajwa kuhusu paja.”

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas, Jarhad na Muhammad bin Jahsh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Paja ni uchi.”

Anas amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifunua paja lake.”

Hadiyth ya Anas cheni yake ya wapokezi imeungana na Hadiyth ya Jarhad ni yenye kuchukua tahadhari zaidi ili kutoka nje ya makinzano.”

Swahiyh al-Bukhaariy pamoja na ”al-Fath” (1/478).

Maafikiano aliyotaja Shaykh yamenukuliwa na Ibn Qudaamah katika ”al-Mughniy” (2/284) kutoka kwa Ibn ´Abdil-Barr.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 26/05/2026