Ikiwa mwenye kuswali ataweka zulia juu ya ardhi yenye najisi au chini ya ardhi anayoswalia ziko sehemu za haja au njia za maji yenye najisi, basi swalah yake ni sahihi kwa kuwa haijagusana moja kwa moja na najisi hiyo. Ibn Kathiyr ametaja katika mnasaba wa maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ

“Na nguo zako zitwaharishe!”[1]

hali ya kunukuu kutoka kwa kundi la Salaf kuhusu tafsiri ya Aayah hii kwa maana ya kujitwahirisha na madhambi na maasi. Kisha akasema: “Muhammad bin Siyriyn amesema:

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ

“Na nguo zako zitwaharishe!”

Kwa maana zioshe kwa maji.”

Ibn Zayd amesema: ”Washirikina hawakuwa wakitwaharika, basi Allaah (´Azza wa Jall) akamwamuru ajitwaharishe na azitwaharishe nguo zake.”

Hili ndilo lililochaguliwa na Ibn Jariyr. Huenda Aayah ikakusanya yote hayo pamoja na usafi wa moyo, kwani waarabu walikuwa wakitumia neno ´nguo` wakikusudia moyo na mwenendo.”

[1] 74:04

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 26/05/2026