Huu ndio mwenendo wa maimamu wa Salaf, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, katika suala hili na masuala mengine yote ya kidini. Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) alitoa mukhtasari wa mbinu yao aliposema:
“Maimamu wa Salaf na wafuasi wao walikuwa wakizitaja Aayah kisha wanazifuatishia kwa Hadiyth zinazoafikiana. Hivo ndivo alivofanya al-Bukhaariy na watangulizi wake na wale waliokuja baada yake katika wale walioandika vitabu vya ´Aqiydah. Imaam Ahmad, Ishaaq bin Raahuuyah na wengine wamemjengea hoja juu ya usahihi wa yale yaliyomo ndani ya Hadiyth kuhusu kushuka kwa Allaah, kuonekana, maneno, uso, mikono na kuja kwa yale ambayo tayari yamo ndani ya Qur-aan. Walithibitisha kuafikiana kwa dalili za Qur-aan na Sunnah na kwamba zinatokana na chemchem moja. Hakuna yeyote, ambaye yuko na elimu na imani ijapo kidogo, anayepinga jambo hilo.
Maana za Qur-aan zinaweza kuthibitishwa tu kupitia yale ambayo wapokezi wa kuaminika wamesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Wao walikuwa ndio warithi wa Mitume. Kisha wanayafuatishia kwa yale yaliyosemwa na Maswahabah na wafuasi wao ambao ndio viongozi wa uongofu.
Je, ni jambo lenye kujificha kwa mtu mwenye akili timamu kwamba kufasiri Qur-aan namna hii ndio bora kuliko tafsiri inayotokana na viongozi wa upotovu na wakuu wa Jahmiyyah na Mu´tazilah, kama vile al-Mariysiy, al-Jubbaa-iy, an-Nadhdhwaam, al-‘Allaaf na mfano wao, ambao wamezua ndani ya Uislamu mambo mapya na Bid´ah, wakaleta mipasuko ndani ya dini yao na wakaanzisha mapote ambapo kila mmoja akawa anafurahika kwa yale aliyomo? Ikiwa haijuzu kuifasiri Qur-aan na kuthibitisha yale yanayofahamishwa nayo na kupata elimu na yakini kupitia Sunnah zilizosihi na zilizothibitishwa za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa maneno ya Maswahabah na wanafunzi wao, itafaa kurejesha maana za Qur-aan kwenye upotoshaji wa Jahm na wafuasi wake na tafsiri mbovu za al-‘Allaaf, an-Nadhdhwaam, al-Jubbaa-iy, al-Mariysiy, ‘Abdul-Jabbaar na vipofu wao na wafuasi mabubu, walio mbali kabisa na Qur-aan na Sunnah na wasiojulikana miongoni mwa wenye elimu na waumini?”[1]
[1] Mukhtaswar-us-Swawaa´iq al-Mursalah, uk. 456.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 50-51
- Imechapishwa: 01/12/2025
Huu ndio mwenendo wa maimamu wa Salaf, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, katika suala hili na masuala mengine yote ya kidini. Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) alitoa mukhtasari wa mbinu yao aliposema:
“Maimamu wa Salaf na wafuasi wao walikuwa wakizitaja Aayah kisha wanazifuatishia kwa Hadiyth zinazoafikiana. Hivo ndivo alivofanya al-Bukhaariy na watangulizi wake na wale waliokuja baada yake katika wale walioandika vitabu vya ´Aqiydah. Imaam Ahmad, Ishaaq bin Raahuuyah na wengine wamemjengea hoja juu ya usahihi wa yale yaliyomo ndani ya Hadiyth kuhusu kushuka kwa Allaah, kuonekana, maneno, uso, mikono na kuja kwa yale ambayo tayari yamo ndani ya Qur-aan. Walithibitisha kuafikiana kwa dalili za Qur-aan na Sunnah na kwamba zinatokana na chemchem moja. Hakuna yeyote, ambaye yuko na elimu na imani ijapo kidogo, anayepinga jambo hilo.
Maana za Qur-aan zinaweza kuthibitishwa tu kupitia yale ambayo wapokezi wa kuaminika wamesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Wao walikuwa ndio warithi wa Mitume. Kisha wanayafuatishia kwa yale yaliyosemwa na Maswahabah na wafuasi wao ambao ndio viongozi wa uongofu.
Je, ni jambo lenye kujificha kwa mtu mwenye akili timamu kwamba kufasiri Qur-aan namna hii ndio bora kuliko tafsiri inayotokana na viongozi wa upotovu na wakuu wa Jahmiyyah na Mu´tazilah, kama vile al-Mariysiy, al-Jubbaa-iy, an-Nadhdhwaam, al-‘Allaaf na mfano wao, ambao wamezua ndani ya Uislamu mambo mapya na Bid´ah, wakaleta mipasuko ndani ya dini yao na wakaanzisha mapote ambapo kila mmoja akawa anafurahika kwa yale aliyomo? Ikiwa haijuzu kuifasiri Qur-aan na kuthibitisha yale yanayofahamishwa nayo na kupata elimu na yakini kupitia Sunnah zilizosihi na zilizothibitishwa za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa maneno ya Maswahabah na wanafunzi wao, itafaa kurejesha maana za Qur-aan kwenye upotoshaji wa Jahm na wafuasi wake na tafsiri mbovu za al-‘Allaaf, an-Nadhdhwaam, al-Jubbaa-iy, al-Mariysiy, ‘Abdul-Jabbaar na vipofu wao na wafuasi mabubu, walio mbali kabisa na Qur-aan na Sunnah na wasiojulikana miongoni mwa wenye elimu na waumini?”[1]
[1] Mukhtaswar-us-Swawaa´iq al-Mursalah, uk. 456.
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 50-51
Imechapishwa: 01/12/2025
https://firqatunnajia.com/29-njia-sahihi-tu-ya-kuifahamu-qur-aan/