29. Allaah anazungumza maneno kikweli

27 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) amesema: “Mimi niko vile mja Wangu anavyonidhania na Mimi ni pamoja Naye anaponitaja. Akinitaja kwenye nafsi yake Nami namtaja kwenye nafsi Yangu, akinitaja katika kundi, Nami namtaja katika kundi ambalo ni bora kuliko wao, akijikurubisha Kwangu paa moja Nami najikurubisha kwake dhiraa, akijikurubisha Kwangu dhiraa Nami najikurubisha kwake kwa kiasi cha kunyoosha mkono hadi kati ya kifuwa na akinijia kwa mwendo mdogo basi Mimi nitamjia kwa kuchapuka.”[1]

Hadiyth hii ni Swahiyh. Kuna tofauti kati ya mazungumzo ya ndani ya nafsi na mazungumzo yenye kusikiwa. Yeye (Ta´ala) anazungumza kwa njia zote mbili. Yeye ndiye ambaye alimzungumzisha Muusa maneno ya kweli, akamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.

[1] al-Bukhaariy (7405), Muslim (2675), Ahmad (2/251, 413 na 480) na at-Tirmidhiy, ambaye ameisahihisha. Ahmad pia amepokea mfano wake kupitia njia tatu kutoka kwa Abu Hurayrah. Ibn Mandah ameipokea katika “Kitaab-ut-Tawhiyd” na pia Hadiyth yenye kuitia nguvu kutoka kwa Anas.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 94-95
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy