Swali 28: Je, inafaa kumswalia na kumtakia amani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi imamu anapotoa Khutbah na akamtaja[1]?

Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapotajwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Khutbah ya ijumaa, Khutbah ya ´iyd na vikao vya Dhikr. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ameangukia pua yule ambaye nitatajwa mbele yake asiniswalie.”[2]

Swalah na amani ziwe juu yake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/338).

[2] at-Tirmidhiy (3468) na Ahmad (7139).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 68
  • Imechapishwa: 01/12/2021