28. Kitu bora unachoweza kuweka kama ´Aqiydah kwa ajili ya Aakhirah

Imaam Abul-Hasan Muhammad bin ´Abdil-Malik al-Karajiy amesema, swahiba wake na Shaykh-ul-Islaam, katika ´Aqiydah yake ambayo aliianza kwa maneno haya:

Uzuri wa mwili wangu ulibadilishwa kwa  mapungufu

na mvi zangu zikachanganyika na ugeni wa wapenzi

Bora ya bekwa ya Aakhirah ni ´Aqiydah

katika njia ya ukweli na subira isiyo na upotofu

´Aqiydah ya Ahl-ul-Hadiyth imeinuliwa kwa watu wa dini ya Allaah

ikafikia daraja tukufu zaidi

´Aqiydah yao ni kwamba Allaah kwa dhati Yake yuko juu ya ´Arshi

pamoja na utambuzi Wake juu ya mambo yote yaliyofichikana

Na kwamba kulingana kwa Mola kunafahamika kwa upande wa akili

lakini namna yake haijulikani kama vile nyota zisivyoeleweka

Imaam na mtambuzi Abu Muhammad ´Abdul-Qaadir bin Abiy Swaalih al-Jiyliy amesema:

”Yeye yuko upande wa juu, amelingana juu ya ´Arshi. Ni mwenye ufalme wa kila kitu na ujuzi Wake umekizunguka kila kitu:

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake linapanda neno zuri na tendo zuri hulitukuza.”[1]

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ

”Malaika na Roho wanapanda Kwake katika siku kipimo chake ni sawa na miaka elfu khamsini.”[2]

Haijuzu kumuelezea kwamba Yuko kila mahali. Bali inasemwa kuwa Yuko juu ya mbingu juu ya ´Arshi, kama Alivyosema Mwenyewe:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[3]

Inapasa kutaja sifa ya kulingana juu kwa maana yake ya wazi bila ya kupindisha maana. Inahusiana na kulingana kwa dhati juu ya ´Arshi. Kitendo Chake (Subhaanahu wa Ta´ala)  kuwa juu ya ´Arshi ni jambo limetajwa ndani ya kila kitabu kilichoteremshwa kwa kila Mtume aliyetumilizwa. Hata hivyo sifa hiyo haitakiwi kufanyiwa namna.”[4]

Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, Mola wa walimwengu wote. Swalah na salamu zimshukie Muhammad, jamaa zake na Maswahabah wake wote. Allaah anatutosheleza na Yeye ndiye mbora wa kutegemewa. Hapana nguvu wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah, Aliye juu, Mtukufu.

[1] 35:10

[2] 70:4

[3] 20:5

[4] al-Ghunyah (1/71).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 87-88
  • Imechapishwa: 31/12/2025