28. Aina za wenye kutenzwa nguvu juu ya ukafiri na hukumu zao

Swali 28: Tunaomba tafsiri ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):

مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّـهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِين

”Atakayemkufuru Allaah baada ya kuamini kwake [atachukuliwa hatua] – isipokuwa yule aliyelazimishwa na huku moyo wake ukawa umetua juu ya imani. Lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao watapata ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kubwa. Hivyo kwa sababu wao wamefadhilisha maisha ya dunia kuliko ya Aakhirah na kwamba Allaah hawaongoi watu makafiri.”[1]

Tunaomba tafsiri ya ufafanuzi wa kina wa Aayah hii pamoja na kuelezea hukumu ya kutenzwa nguvu.

Jibu: Katika Aayah hii Allaah amebainisha ya kwamba yule ambaye atamkufuru Allaah baada ya imani yake, basi atapata ghadhabu na adhabu kuu ya Allaah. Hii ni kwa sababu ameamua kupendelea maisha ya duniani kuliko ya Aakhirah. Aayah inamkusanya pia:

1 – Mwenye kumkufuru Allaah kwa kumaanisha kweli na kwa khiyari.

2 – Mwenye kumkufuru Allaah kwa mzaha, kimchezo na kwa maskhara.

3 – Mwenye kumkufuru Allaah kwa kuogopa.

4 – Mwenye kumkufuru Allaah kwa kutenzwa nguvu lakini moyo wake umetua juu ya kufuru.

Kwa sababu Allaah hakumbagua kutokana na ukafiri isipokuwa ambaye amefanya kufuru kwa kutenzwa nguvu na wakati huohuo moyo wake umetua juu ya imani. Isitoshe Allaah amebainisha ya kwamba – tukitoa aina hii ya mwisho ya watu – anakuwa kafiri kwa sababu ni aina nyenginezo ni watu wameyapa kipaumbele maisha ya dunia mbele ya maisha ya Aakhirah. Kwa hivyo mwenye kumkufuru Allaah kwa makusudi hakika ameyapa kipaumbele maisha ya duniani mbele ya maisha ya Aakhirah. Mwenye kumkufuru Allaah kwa mzaha hakika ameyapa kipaumbele maisha ya duniani mbele ya maisha ya Aakhirah. Mwenye kumkufuru kwa kuogopa hakika ameyapa kipaumbele maisha ya duniani mbele ya maisha ya Aakhirah. Mwenye kumkufuru kwa kulazimishwa na wakati huohuo moyo wake ukatulizana juu ya kufuru, hakika ameyapa kipaumbele maisha ya duniani mbele ya maisha ya Aakhirah. Amesema (Ta´ala):

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِين

”Hivyo kwa sababu wao wamefadhilisha maisha ya dunia kuliko ya Aakhirah na kwamba Allaah hawaongoi watu makafiri.”

Allaah hatowahidi kutokana na ukafiri na upotofu wao. Tunamuomba Allaah hifadhi.

[1] 16:106

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 62-64
  • Imechapishwa: 09/01/2026