Inafaa kwa mwanamke kutumia vitu vinavyozuia hedhi kwa kutimia masharti mawili:

1- Asichelei kupata madhara yoyote. Itakuwa haijuzu lau kitu hicho kitakuwa na madhara kwake. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ

“Wala msijitupe kwa mikono yenu katika maangamizi.” (02:195)

وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ

“Wala msijiue.” (04:29)

2- Mume atoe ruhusa yake ikiwa yanamuhusu. Mfano wa hilo apate ada yake pale ambapo ni wajibu kwake kumhudumia. Mwanamke anatumia dawa kurefusha ada yake ili aweze kupata matumizi zaidi. Katika hali hii haifai kwake kufanya hivi bila ya idhini yake. Mfano mwingine ni kutumia dawa ili kuzuia mimba. Hapa pia anatakiwa kumuomba idhini mume.

Hata kama inafaa kutumia dawa hizi, bora ni kutofanya hivo ikiwa hakuna haja. Afya zaidi ni kuyaacha maumbile kama jinsi yalivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016