Miongoni mwa adabu zake ni kwamba avumilie ukali wa mwalimu na tabia yake mbaya. Hilo lisimzuilie kuendelea kuwa naye na kuamini ukamilifu wake. Ayatafsiri matendo na maneno yake ambayo kwa nje yanaonekana kuwa na kasoro kwa tafsiri sahihi. Hakuna anayeshindwa kufanya hivyo isipokuwa mwenye tawfiyq kidogo au asiye na tawfiyq kabisa. Ikiwa mwalimu atamfanyia ukali, basi aanze yeye kumuomba radhi mwalimu na aonyeshe kuwa kosa ni lake na lawama iko juu yake. Kwani hilo lina manufaa zaidi kwake duniani na Aakhirah na ni lenye kusafisha zaidi moyo wa mwalimu. Walikuwa wakisema:
”Asiyesubiri juu ya udhalili wa kujifunza, ataishi maisha yake katika upofu wa ujinga. Anayesubiri juu yake, mwisho wake utakuwa ni heshima ya Aakhirah na dunia.”
Masimulizi yanayotambulika ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) yanasema:
”Nilijinyenyekeza nikiwa mtafutaji wa elimu ambapo nikawa mwenye kuheshimiwa nikiwa ninayetafutwa.”
Amesema vyema aliyesema:
Asiyeonja ladha ya unyenyekevu kwa muda mfupi
ataishi maisha yake yote katika udhalili
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 36
- Imechapishwa: 26/08/2026
Miongoni mwa adabu zake ni kwamba avumilie ukali wa mwalimu na tabia yake mbaya. Hilo lisimzuilie kuendelea kuwa naye na kuamini ukamilifu wake. Ayatafsiri matendo na maneno yake ambayo kwa nje yanaonekana kuwa na kasoro kwa tafsiri sahihi. Hakuna anayeshindwa kufanya hivyo isipokuwa mwenye tawfiyq kidogo au asiye na tawfiyq kabisa. Ikiwa mwalimu atamfanyia ukali, basi aanze yeye kumuomba radhi mwalimu na aonyeshe kuwa kosa ni lake na lawama iko juu yake. Kwani hilo lina manufaa zaidi kwake duniani na Aakhirah na ni lenye kusafisha zaidi moyo wa mwalimu. Walikuwa wakisema:
”Asiyesubiri juu ya udhalili wa kujifunza, ataishi maisha yake katika upofu wa ujinga. Anayesubiri juu yake, mwisho wake utakuwa ni heshima ya Aakhirah na dunia.”
Masimulizi yanayotambulika ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) yanasema:
”Nilijinyenyekeza nikiwa mtafutaji wa elimu ambapo nikawa mwenye kuheshimiwa nikiwa ninayetafutwa.”
Amesema vyema aliyesema:
Asiyeonja ladha ya unyenyekevu kwa muda mfupi
ataishi maisha yake yote katika udhalili
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 36
Imechapishwa: 26/08/2026
https://firqatunnajia.com/27-subira-ya-mwanafunzi-kwa-mwalimu/