Miongoni mwa mambo yanayosisitizwa kupewa umuhimu ni kwamba asisome kwa mwalimu katika hali ya kuwa moyo wa mwalimu umeshughulika, amechoka, amechukizwa, ameingiwa na khofu, huzuni, furaha, kiu, usingizi, wasiwasi na mfano wa hayo yanayomletea uzito au yanayomzuia kuwa na uwepo kamili wa moyo na uchangamfu. Aidha atumie vizuri nyakati za uchangamfu wake.

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 35
  • Imechapishwa: 26/08/2026