27. Ni vipi maiti anavikwa sanda kwa nisba ya mwanamme na mwanamke?

Swali 27: Ni vipi maiti anavikwa sanda kwa nisba ya mwanamme na mwanamke[1]?

Jibu: Sunnah ni mwanamme avikwe sanda ndani ya nguo tatu nyeupe. Hivo ndivo alivovikwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Itatosha pia akivikwa sanda ndani ya nguo moja pana na inayomuenea na kumsitiri vizuri. Itafaa vilevile akivikwa sanda ndani ya kanzu, shuka ya chini na shuka kubwa anayozingirwa ndani yake.

Kuhusu mwanamke bora ni kumkafini ndani ya nguo tano; shuka ya chini, shungi, kanzu na mashuka mawili makubwa anayozingirwa ndani yake. Hivi ndivo bora, kama walivosema wanazuoni. Kumepokelewa Hadiyth kuhusu hayo zinazofahamisha mambo hayo. Hapana neno pia akikafiniwa ndani ya chache kuliko hizo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/127).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 25
  • Imechapishwa: 17/12/2021