25. Inafaa kwa mwoshaji maiti kubainisha baadhi ya alama za kheri na shari?

Swali 25: Inafaa kwa mwoshaji maiti kubainisha baadhi ya alama za kheri na shari[1]?

Jibu: Alama za kheri ni sawa kuzibainisha. Kuhusu alama za shari haifai. Kwa sababu kufanya hivo ni usengenyi. Lakini ni sawa endapo atasema baadhi ya wafu wanakuwa weusi au vyenginevyo. Kilichokatazwa ni pale atapolenga kwa kutaja jina na kwamba ameona kadhaa miongoni mwa alama za shari. Kwa sababu kufanya hivo kutawahuzunisha familia yake na kuwaudhi. Isitoshe ni katika kusengenya.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/123).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 24
  • Imechapishwa: 17/12/2021