27. Mwenye furaha na mla khasara kwenye matumbo ya mama zao

Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

49 – Aliye na furaha ni yule anayefurahishwa na mipango ya Allaah, aliyekula khasara ni yule asiyefurahishwa na mipango ya Allaah.

MAELEZO

Hii ni maana ya Hadiyth aliyoipokea al-Bazzaar na wengineo kupitia kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

”Mla khasara ni yule aliyekula khasara tumboni mwa mama yake, na aliye na furaha ni yule aliyefurahi tumboni mwa mama yake.”

Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh, kama nilivyobainisha katika ”ar-Rawdhw an-Nadhwiyr” (1098) na “Dhwilaal-ul-Jannah fiy Takhriyj-is-Sunnah” (188).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 41
  • Imechapishwa: 24/09/2024