27. Msafiri anayejiunga na imamu katika Tashahhud ya kwanza

Swali 27: Nilikuwa msafiri na katika moja ya mapumziko yangu ilinipata swalah ya Dhuhr katika msikiti wa Istiraahah na walikuwa wenye kuswali kwa kukamilisha. Nilipoingia ndani ya swalah imamu alikuwa katika Tashahhud ya kwanza na wakati imamu alipotoa salamu nikatoa naye salamu kwa sababu nilikuwa msafiri. Je, kitendo changu hichi ni cha sawa? Mambo yakiwa ni kinyume na hivyo niirudie swalah yangu[1]?

Jibu: Ni lazima kwako kuirudia swalah yako. Kwa sababu kilicho cha wajibu kwa msafiri anaposwali nyuma ya mkazi basi aswali Rak´ah nne. Hivo ndivo ilivyosihi Sunnah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/263).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 42
  • Imechapishwa: 09/03/2022