27. Kumtakasa Allaah kutokana na mtoto na baba

Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

وليس بمولودٍ وليس بوالدٍ

07 – Hana mtoto wala Hana baba

وليس له شِبْهٌ تعالى المُسبحُ

     na wala hana mfanano – Ametakasika msabihiwaji

MAELEZO

Haya yamechukuliwa kutoka katika maneno ya Allaah (Ta´ala) katika Suurah “al-Ikhaasw”:

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Sema: “Yeye ni Allaah Mmoja pekee. Allaah ndiye mkusudiwa. Hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala hakuna yeyote anayefanana na kulingana Naye.” (112:01-04)

Imeitwa kuwa ni Suurah “al-Ikhaasw” kwa kuwa imeitakasa Tawhiyd. Qur-aan imegawanyika sehemu tatu:

1 – Tawhiyd. Maelezo kuhusu Allaah, kumwabudu na makatazo ya kumshirikisha.

2 – Maamrisho na makatazo Yake. Ni yale ya halali na haramu na hukumu za Kishari´ah.

3 – Maelezo juu ya Mitume, nyumati, yaliyotangulia na yaliyoko mbele, Pepo na Moto.

Suurah hii imetakasa aina ya kwanza ambapo ni maelezo juu ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). Ni kuhusu Tawhiyd. Ndio maana ikawa ni sawa na theluthi ya Qur-aan inapokuja katika fadhilah[1]. Kwa sababu imetakasa kumpwekesha Allaah (´Azza wa Jall). Hii ndio sababu ikaitwa Suurah “al-Ikhaasw”. Ndani yake mna makanusho na mathibitisho. Inamkanushia Allaah kuwa na mapungufu na wakati huohuo inamthibitishia Allaah (Jalla wa ´Alaa) ukamilifu:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: “Yeye ni Allaah Mmoja pekee.”

Haya ni mathibitisho.

اللَّـهُ الصَّمَدُ

“Allaah ndiye mkusudiwa.”

Haya ni mathibitisho.

لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“Hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala hakuna yeyote anayefanana na kulingana Naye.”

Haya ni makanusho. Amejikanushia mapungufu na wakati huohuo akajithibitishia ukamilifu. Maneno Yake:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: “Yeye ni Allaah Mmoja pekee.”

Bi maana ni mmoja asiyekuwa na mshirika si katika uola, kuabudiwa wala katika majina na sifa Zake. Ni Mmoja pekee katika vigawanyo vitatu vya Tawhiyd. Maneno Yake:

اللَّـهُ الصَّمَدُ

“Allaah ndiye mkusudiwa.”

Bi maana anayekusudiwa na viumbe na wanaomba kutoka Kwake haja mbalimbali. Kisha akakanusha na kusema:

لَمْ يَلِدْ

“Hakuzaa… “

Bi maana hana mtoto. Hakika Yeye (Subhaanah) ametakasika kutokamana na kuwa na mtoto.

[1] al-Bukhaariy (5013).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 83-84
  • Imechapishwa: 09/01/2024