Wanaamini Hodhi na Kawthar, kwamba lipo kundi litakaloingia Peponi bila ya hesabu wala adhabu, kwamba baadhi yao watafanyiwa hesabu nyepesi na baada ya hapo waingie Peponi, pasi na kitu kibaya wala adhabu itakayowapata, na kwamba kuna kundi la watenda madhambi miongoni mwao litakaloingia Motoni kisha baadaye waachwe huru, watolewe nje na kukutanishwa na ndugu zao ambao tayari walikwishawatangulia huko. Hawatodumishwa Motoni milele. Kuhusu makafiri, wao watadumishwa humo milele. Kamwe hawatotoka humo. Allaah hatomwacha kabisa ndani yake mtenda dhambi yeyote katika waumini.
- Muhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 263
- Imechapishwa: 13/12/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)