Akifa yule ambaye anadaiwa funga ya kafara (kama mfano wa funga ya ambaye amemfananisha mke wake na mama yake), basi atatolewa chakula kumpa masikini kwa kila siku moja. Hatofungiwa. Garama za chakula hicho zitatolewa katika mirathi yake. Kwa sababu swawm haikuwa inakubali kukaliwa naibu kipindi cha uhai wake. Basi vivyo hivyo baada ya kufa kwake. Hayo ndio maoni ya wanachuoni wengi.

Akifa yule ambaye anadaiwa swawm ya nadhiri, basi inapendekeza kwa yule walii wake kumfungia. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kwamba kuna mwanamke alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Mama yangu amefariki na anadaiwa funga ya nadhiri. Je, nimfungie?” Akajibu: “Ndio.”

Walii ni wale wanaomrithi.

Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Nadhiri mtu anafungiwa pasi na ile funga ambayo msingi wake ni faradhi. Haya ndio maoni ya Ahmad na wengine. Pia kuna maandiko kutoka kwa Ibn ´Abbaas na ´Aaishah. Isitoshe ndio jambo linalopelekea katika dalili na kipimo. Kwa sababu kimsingi wa dini nadhiri sio kitu cha lazima. Ni kitu ambacho mja mwenyewe amejiwajibishia. Kwa hiyo ikawa katika ngazi ya dini. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaifananisha na dini.

Kuhusu swawm ambayo msingi wake Allaah ndiye ameifaradhisha ni moja katika nguzo za Uislamu. Kwa hivyo si yenye kukaliwa niaba kwa hali yoyote. Ni kama ambavo swalah na shahaadah havikaliwi niaba. Kwani malengo ya viwili hivyo ni mja kutii  yeye kama yeye na kutekeleza haki ya uja ambayo Allaah amemuumba kwa ajili yake na akamwamrisha, kitu ambacho hakuna mwengine awezaye kumtekelezea kama ambavo hakuna mwengine awezaye kumswalia.”

Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Atalisha kwa kila siku moja masikini. Hivo ndivo alivoonelea Ahmad, Ishaaq na wengineo. Ndivo ambavo mtazamo unavopelekea kama ambavo yanawajibisha mapokezi. Nadhiri ilikuwa yenye kuthibiti katika dhimma yake na hivyo ataifanya hata baada ya kufa kwake. Kuhusu kufunga Ramadhaan Allaah hajamuwajibishia yule asiyeweza. Bali amemwamrisha yule asiyeweza kutoa fidia ya kumlisha masikini. Kulipa kunamuhusu yule mwenye kuweza na si kwa yule asiyeweza. Kwa hiyo hakuna haja ya yeyote kumlipia mwengine. Lakini funga ya nadhiri na vyenginevyo vilivyowekewa nadhiri atafanya hivo pasi na tofauti kutokana na Hadiyth ambazo Swahiyh.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/388-389)
  • Imechapishwa: 06/04/2021