05. Hadiyth “Mimi ndiye wa kwanza nitakayeidhinishwa kusujudu… “

180 – Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi ndiye wa kwanza nitakayeidhinishwa kusujudu siku ya Qiyaamah na mimi ndiye wa kwanza nitakayenyanyua kichwa. Nitaangalia mbele yangu na nitaujua Ummah wangu kati ya nyumati zengine. Nyuma yangu itakuwa mfano wa hivo, upande wangu wa kulia itakuwa mfano wa hivo, upande wangu wa kushoto itakuwa mfano wa hivo.” Akasema bwana mmoja: “Ni vipi utaujua Ummah wako, ee Mtume wa Allaah, kuanzia kwa Nuuh mpaka kwa Ummah wako?” Akasema: “Watakuwa na mabaka na wenye viungo vyenye kung´aa kutokana na athari ya wudhuu´. Hakuna mwengine atakayekuwa nayo zaidi yao. Nitawatambua pia pale watakapokuja na madaftari yao kwa mikono yao ya kuume na vizazi vyao vitakuwa vikipita mbele yao.”[1]

Ameipokea Ahmad. Katika cheni ya wapokezi yupo Ibn Lahiy´ah. Kwa vile Hadiyth imepokelewa kupitia njia zengine ni nzuri.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/187-188)
  • Imechapishwa: 05/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy