26. Wanafunzi wanaacha kusoma ili wasije kubeba majukumu makubwa

Swali 26: Baadhi ya wanafunzi walioanza kutafuta elimu wanaingiwa na fikira za kwamba kadiri wanavyokwenda katika darsa ndio jinsi wanavyobeba majukumu makubwa katika kuifikisha elimu na kuitendea kazi. Jambo ambalo huwafanya baadhi kujichomoa na kutafuta elimu ya Kishari´ah. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Huu ni wasiwasi wa shaytwaan. Anakushawishi kwamba usijifunze ili elimu isije kuwa hoja dhidi yako.

Hata hivyo kubaki katika ujinga pamoja na kuwa wanazuoni wanapatikana si ni hoja dhidi yako pia? Kule kubaki katika ujinga ilihali elimu, wanazuoni na darsa zipo ni khatari zaidi kuliko kwenda katika darsa na kusoma na katika matukio fulani pengine usitendee kazi yale uliyojifunza. Ni jambo la kimaumbile mwanaadamu kufanya upungufu katika matendo na kutenda dhambi kadhaa. Kunatarajiwa kwake kuzindukana, kutubia dhambi zake na kujirekebisha pale anapoenda katika vikao na darsa za wanachuoni misikitini. Mizunguko hii ya kielimu inazihuisha nyoyo. Usimwache shaytwaan akakukosesha elimu yenye manufaa na kujifunza elimu ya Kishari´ah kutokana na shubuha na wasiwasi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 31/05/2023
  • mkusanyaji: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy