Mja anaposimama katika swalah basi shaytwaan huona wivu mkubwa kwake. Kwani amesimama katika nafasi tukufu zaidi, ya karibu zaidi, yenye kumkasirisha zaidi shaytwaan na yenye kumuumiza zaidi kwake. Hivyo shaytwaan hujitahidi na kujituma ili asimamishe mja katika nafasi hiyo. Bali haachi kumuahidi, kumtamkia matarajio na kumsahaulisha na humiminia majeshi yake ya farasi na miguu, mpaka humfanya achukulie swalah kuwa jambo dogo, kisha humfanya aichezee na mwishowe aiiache kabisa.
Ikiwa shaytwaan atashindwa kufanya hivyo ambapo mja akamwasi, kisha akasimama katika nafasi hiyo ya swalah, basi adui wa Allaah huja kumkabili ambapo akaanza kutembea baina yake na nafsi yake na huweka kizuizi baina yake na moyo wake. Matokeo yake humsababishia kukumbuka ndani ya swalah kile ambacho hakuwa anakikumbuka kabla ya kuingia ndani yake. Hata huenda alishasahau jambo fulani au haja fulani na alikuwa amekata tamaa nayo, lakini humkumbusha ndani ya swalah ili amshughulishe moyo wake na kuondoa uhusiano kati yake na Allaah (´Azza wa Jall). Basi husimama katika swalah bila ya moyo. Kwa hivyo hapati kutoka kwa kuelekea kwa Allaah wala heshima Yake wala ukaribu Wake kile ambacho hupata mwenye kumuelekea Mola wake (´Azza wa Jall) kwa moyo wake katika swalah yake. Hutoka katika swalah yake kama alivyoingia ndani yake – pamoja na madhambi yake, makosa yake na mizigo yake – ambayo haikupunguzwa na swalah.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 45
- Imechapishwa: 06/08/2025
Mja anaposimama katika swalah basi shaytwaan huona wivu mkubwa kwake. Kwani amesimama katika nafasi tukufu zaidi, ya karibu zaidi, yenye kumkasirisha zaidi shaytwaan na yenye kumuumiza zaidi kwake. Hivyo shaytwaan hujitahidi na kujituma ili asimamishe mja katika nafasi hiyo. Bali haachi kumuahidi, kumtamkia matarajio na kumsahaulisha na humiminia majeshi yake ya farasi na miguu, mpaka humfanya achukulie swalah kuwa jambo dogo, kisha humfanya aichezee na mwishowe aiiache kabisa.
Ikiwa shaytwaan atashindwa kufanya hivyo ambapo mja akamwasi, kisha akasimama katika nafasi hiyo ya swalah, basi adui wa Allaah huja kumkabili ambapo akaanza kutembea baina yake na nafsi yake na huweka kizuizi baina yake na moyo wake. Matokeo yake humsababishia kukumbuka ndani ya swalah kile ambacho hakuwa anakikumbuka kabla ya kuingia ndani yake. Hata huenda alishasahau jambo fulani au haja fulani na alikuwa amekata tamaa nayo, lakini humkumbusha ndani ya swalah ili amshughulishe moyo wake na kuondoa uhusiano kati yake na Allaah (´Azza wa Jall). Basi husimama katika swalah bila ya moyo. Kwa hivyo hapati kutoka kwa kuelekea kwa Allaah wala heshima Yake wala ukaribu Wake kile ambacho hupata mwenye kumuelekea Mola wake (´Azza wa Jall) kwa moyo wake katika swalah yake. Hutoka katika swalah yake kama alivyoingia ndani yake – pamoja na madhambi yake, makosa yake na mizigo yake – ambayo haikupunguzwa na swalah.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 45
Imechapishwa: 06/08/2025
https://firqatunnajia.com/26-shaytwaan-wakati-mja-anaposimama-kuswali/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket