2 – Kuendelea kufunga kunafaa ikiwa mtu anaweza kufanya hivyo. Hili limepokelewa kutoka kwa ´Abdullaah bin az-Zubayr. Ibn Abiy Shaybah amesimulia kuwa aliendelea kufunga siku kumi na tano[1]. Pia imepokelewa kutoka kwa Abu Sa’iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) kuwa amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuendelea kufunga bila kufuturu na huyu dada yangu anaendelea kufunga nami namkataza.”[2]
Maoni haya yamechukuliwa na kundi katika Salaf kama vile Abdur-Rahmaan bin Abi Nu’aym, Ibraahiym bin Yaziyd at-Taymiy, ‘Aamir bin ´AbdullaAh bin az-Zubayr, Abu al-Jawzaa´ na wengineo[3]. Hawa wametumia dalili kwamba kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliendelea kufunga na Maswahabah wake kwa siku moja, kisha siku nyingine hadi walipoona mwezi mwandamo. Lau kama katazo hilo lingekuwa la uharamu, basi asingefunga pamoja nao wala asingewaacha wafanye hivyo, bali angaliwakataza. Abu Daawuud amepokea kupitia kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa kwamba mtu mmoja miongoni mwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuumikwa na kuunganisha swawm, lakini hakuwaharamishia Maswahabah zake kufanya hivo[4]… Swahabah huyo ameweka wazi kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuharamisha kuunganisha swalah, jambo linalojulisha kuwa katazo hilo halikuwa kwa ajili ya uharamu na kwamba inachukiza tu kama huruma kwao na kuwafanyia wepesi. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuunganisha swawm kwa ajili ya kuwahurumia…”[5]
Hili ni kama vile alivyowakataza kuswali swalah ya usiku kwa kukhofia kwamba isije kufaradhishwa kwao na wala hakuwakemea wale waliomfuata na kufanya hivyo miongoni mwa wale ambao hawakupata uzito wowote.
[1] al-Muswannaf (03/84) na cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh, kama ilivyo katika “Fath-ul-Baariy” (04/204).
[2] al-Muswannaf (03/82).
[3] Fath-ul-Baariy (04/204).
[4] as-Sunan (2374) na mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh.
[5] al-Bukhaariy (1967) na Muslim (1105).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/36-37)
- Imechapishwa: 11/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)