7 – Kichenguzi cha saba cha wudhuu´: Kumuosha maiti. Wanazuoni wametofautiana kuhusu hukumu ya kutawadha baada ya kumwosha maiti juu ya mitazamo miwili:
1 – Ni wajibu kutawadha.
2 – Inapendeza kutawadha.
Zote mbili zimetajwa na Ibn Qudaamah katika ”al-Mughniy” (1/256) na akayapa nguvu maoni yanayosema kuwa inapendeza. Ameipokea Abu Daawuud (3161) na wengineo kupitia kwa Abu Hurayrah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anayemwosha maiti basi na aoge, na anayembeba basi na atawadhe.”
Ameitaja al-Albaaniy katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (144) na katika kitabu ”Ahkaam-ul-Janaa’iz”, uk. 53. Usahihi wake umenakiliwa kutoka kwa Ibn-ul-Qayyim, Ibn-ul-Qattwaan, Ibn Hazm na Ibn Hajar al-´Asqalaaniy. Akataja kuwa inachukuliwa kama kupendeza na si lazima. Hilo ni kutokana na Hadiyth nzuri juu ya suala hilo kutoka kwa Ibn ´Abbaas na masimulizi kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhum).
Ikiwa anayemuosha maiti atagusa tupu ya maiti bila kizuizi, basi inamlazimu kutawadha kwa sababu ya kugusa tupu, si kwa sababu ya kumwosha maiti. Tazama ”Fataawaa” (10/165) ya Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 28-29
- Imechapishwa: 26/05/2026
7 – Kichenguzi cha saba cha wudhuu´: Kumuosha maiti. Wanazuoni wametofautiana kuhusu hukumu ya kutawadha baada ya kumwosha maiti juu ya mitazamo miwili:
1 – Ni wajibu kutawadha.
2 – Inapendeza kutawadha.
Zote mbili zimetajwa na Ibn Qudaamah katika ”al-Mughniy” (1/256) na akayapa nguvu maoni yanayosema kuwa inapendeza. Ameipokea Abu Daawuud (3161) na wengineo kupitia kwa Abu Hurayrah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anayemwosha maiti basi na aoge, na anayembeba basi na atawadhe.”
Ameitaja al-Albaaniy katika ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (144) na katika kitabu ”Ahkaam-ul-Janaa’iz”, uk. 53. Usahihi wake umenakiliwa kutoka kwa Ibn-ul-Qayyim, Ibn-ul-Qattwaan, Ibn Hazm na Ibn Hajar al-´Asqalaaniy. Akataja kuwa inachukuliwa kama kupendeza na si lazima. Hilo ni kutokana na Hadiyth nzuri juu ya suala hilo kutoka kwa Ibn ´Abbaas na masimulizi kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhum).
Ikiwa anayemuosha maiti atagusa tupu ya maiti bila kizuizi, basi inamlazimu kutawadha kwa sababu ya kugusa tupu, si kwa sababu ya kumwosha maiti. Tazama ”Fataawaa” (10/165) ya Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 28-29
Imechapishwa: 26/05/2026
https://firqatunnajia.com/26-kumuosha-maiti/