26. Kufuata njia ilionyooka na kujiepusha na vichochoro

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Katika al-Bukhaariy imekuja:

“Nitapokuwa nimesimama katika umati wa watu. Pindi nitapowajua nao wanijue atajitokeza mtu kati yetu na kusema: “Njooni!” Niseme: “Kuelekea wapi?” Aseme: “Ninaapa kwa Allaah! Kuelekea Motoni.” Niseme: “Kwani wana nini?” Aseme: “Waliritadi baada yako.” Halafu kuje umati mwingine”, na useme hali kadhalika. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Wachache sawa na idadi ya ngamia walioachwa ndio wataifikia.”[1]

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nitasema kama alivyosema mja mwema:

وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ

“Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao, lakini uliponipaisha juu ulikuwa Wewe ndiye Mwenye kuchunga juu yao; na Wewe juu ya kila jambo ni Mwenye kushuhudia.” (05:117)

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mtoto yeyote isipokuwa huzaliwa katika maumbile. Baada ya hapo wazazi wake ndio humfanya kuwa myahudi, mnaswara au mwabudia moto. Ni kama ambavo mnyama huzaa mnyama mzima; je, mtahisi kuwa hana pembe mpaka nyinyi ndiye mumwondoshe pembe?”  Kisha Abu Hurayrah akasoma:

فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا

“… imani hiyo ndio maumbile Allaah aliyowaumbia watu wote…” (30:30)

Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Watu walikuwa wakimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu mambo ya kheri na mimi nikimuuliza kuhusu mambo ya shari kwa kuchelea yasije kunipata. Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Tulikuwa katika kipindi cha kikafiri na shari na Allaah akatuletea kheri hii. Je, kuna shari baada ya kheri hii?” Akajibu: “Ndio.” Nikasema: “Je, kuna kheri baada ya shari hiyo?” Akajibu: “Ndio, na itakuwa na moshi.” Nikamuuliza: “Ni upi moshi wake?” Akajibu: “Ni watu wenye kufuata isiyokuwa njia na uongofu wangu. Kuna mambo utayokubaliana nayo na mengine utayapinga.” Nikasema: “Kuna shari baada ya kheri hiyo?” Akasema: “Ndio, fitina ya upofu na walinganizi katika milango ya Motoni. Yule mwenye kuwaitikia wanamtupa humo.” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Tueleze nao.” Akasema: “Ni watu wanaotokamana na sisi na wanazungumza lugha yetu.” Nikauliza: “Unaniamrisha nini nikikutana na hilo?” Akasema: “Shikamana na mkusanyiko wa waislamu na kiongozi wao.” Nikasema: “Vipi kukiwa hakuna mkusanyiko wala kiongozi?” Akasema: “Jiepushe na hayo makundi yote hata kama utahitajia kuuma mzizi wa mti mpaka yakufikie mauti.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim ambaye amezidisha:

“Kuna nini baadaye?” Akasema: “Kisha atajitokeza ad-Dajjaal. Atakuwa na mto na moto. Atayetumbukia kwenye moto wake itamuwajibikia kulipwa ujira wake na madhambi yake kufutwa. Na yule mwenye kutumbukia kwenye pepo yake itamuwajibikia kuadhibiwa.” Nikasema: “Kuna nini baadaye?” Akasema: “Halafu kunakuja Qiyaamah.”[3]

Abul-´Aaliyah amesema:

“Jifunzeni Uislamu. Mtapojifunza, msiupe mgongo. Lazimianeni na njia iliyonyooka, kwani hakika ndio Uislamu. Msende kinyume na njia kuliani na kushotoni. Lazimianeni na Sunnah za Mtume wenu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na tahadharini na matamanio haya.”

Yazingatie maneno haya ya Abul-´Aaliyah – ni matukufu kiasi gani! Tambua zama zake ambapo akitahadharisha matamanio ambayo yule mwenye kuyafuata anakuwa ameupa Uislamu mgongo. Ameufasiri Uislamu kuwa ni Sunnah na khofu yake ilikuwa kwa Taabi´uun mabingwa wasiende kinyume na Qur-aan na Sunnah. Hapo ndipo itakubainikia maana ya maneno ya Allaah:

إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ ۖ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ

“Pindi Mola Wake alipomwambia: “Jisalimishe!” Akajibu: “Nimejisalimisha kwa [Allaah], Mola wa walimwengu.” (02:131)

na:

وَوَصَّىٰ بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ

“Na Ibraahiym akawausia hayo wanawe na [kadhalika] Ya’quub [akawaambia]: “Enyi wanangu! Hakika Allaah amekuchagulieni nyinyi dini; hivyo basi msife isipokuwa nyinyi ni waislamu.” (02:132)nja

na:

وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ ۚ وَلَقَدِ اصْطَفَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ

“Na nani atakayejitenga na imani ya Ibraahiym isipokuwa anayeitia nafsi yake upumbavu? Na kwa hakika Tumemteua duniani, naye Aakhirah ni miongoni mwa waja wema.” (02:130)

Izingatie misingi hii mikubwa ambayo ndio misingi ya misingi na ambayo watu wameghafilika nayo. Kwa kuielewa basi itabainika maana ya Hadiyth katika mlango huu na mingineyo.

Kuhusiana na yule mwenye kuisoma ni mamoja hii na mingineyo na huku anajiaminisha kuwa hayawezi kumfika na anafikiria kuwa yanawahusu watu waliokuwepo hapo kale wakatokomea, basi Allaah yuwasema:

أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ

“Je, wameaminisha nja za Allaah? Basi hawaaminishi njama za Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.” (07:99)

Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Siku moja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitupigia msitari kwenye ardhi kisha akasema: “Hii ni njia ya Allaah.” Halafu akapiga vimisitari kuliani na kushotoni kisha akasema: “Hivi ni vichochoro. Kuna Shaytwaan mwenye kuita katika kila kichochoro.” Halafu akasoma:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“Hii ndio njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate vichochoro [vinginevyo]; vikakufarikisheni na njia Yake!”[4] (06:153)

MAELEZO

Haya yanabainisha kuwa muumini anatakiwa kuchukua tahadhari, asidanganyike na wingi na azingatie Sunnah na dalili. Anatakiwa kukhofu juu ya nafsi yake na asijiaminishe. Allaah amesema:

أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ

“Je, wameaminisha nja za Allaah? Basi hawaaminishi njama za Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.”

Mtu anatakiwa kufanya matendo na ajitahidi matendo mema na huku awe ni mwenye khofu na asiwe mwenye utulivu. Bali atahadhari kutokamana na Bid´ah na maasi, awafuate watu wa haki, anyooke pamoja nao, ajiepushe na watu wa batili na kutangamana nao. Hivi ndivo anavokuwa muumini. Daima anakuwa ni mwenye kuchukua tahadhari. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ هُمْ خَيْرُ الْبَرِيَّةِ جَزَاؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًاۖ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ رَبَّهُ

“Hakika wale walioamini na wakafanya mema, basi hao ndio wema kabisa wa viumbe. Malipo yao yako kwa Mola wao; mabustani ya kudumu milele yapitayo chini yake mito hali ya kuwa ni wenye kudumu humo milele. Allaah ataridhika nao, nao wataridhika Naye; hayo ni kwa yule anayemuogopa Mola wake.” (98:07-08)

إِنَّ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ

”Hakika wale wanaomuogopa Mola wao katika hali ya ghaibu watapata msamaha na ujira mkubwa.” (67:12)

فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

“Basi msiwakhofu – na nikhofuni Mimi – mkiwa ni waumini!” (03:175)

وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ

“Kwa wale mwenye kukhofu kusimama mbele ya Mola wake atapata bustani mbili.” (55:46)

Kwa hivyo ni lazima kwa mtu kutahadhari na asiwe na utulivu. Usifuate maoni ya watu mpaka kwanza ujue dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah.

[1] al-Bukhaariy (6587).

[2] al-Bukhaariy (3606) na Muslim (1847).

[3] ´Abdur-Razzaaq katika ”al-Muswannaf” (11/367), al-Marwaziy katika ”as-Sunnah”, uk. 13, al-Laalakaa’iy katika ”Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah (1/56) na Abu Nu´aym (2/218).

[4] an-Nasaa’iy (6/343), Ahmad (1/435), ad-Daarimiy (202) na al-Bazzaar (57113).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 43-46
  • Imechapishwa: 10/11/2020