111 – Muhammad bin Bashshaar ametukhabarisha: Yahyaa bin Sa´iyd ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd: Nimemsikia Sa´iyd bin al-Musayyab akisema: Nimemsikia Sa´d bin Maalik akisema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Uhud alinitajia wazazi wake kwa lengo la kuwatoa fidia kwangu.”[1]

112 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: al-Layth ametukhabarisha … Pia ´Aliy bin Khashram ametukhabarisha: ´Iysaa ametukhabarisha, kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd, kutoka kwa Ibn-ul-Musayyab, kutoka kwa Sa´d, ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Uhud alinitajia wazazi wake na kusema: ”Rusha mshale, watolewe fidia kwako wazazi wangu!”

Qutaybah amesema:

”… wakati alipokuwa anapambana vita.”

Hakutaja ”Rusha mshale”.

113 – ´Amr bin Yahyaa bin al-Haarith ametukhabarisha: Abu Swaalih ametukhabarisha: Abu Ishaaq ametukhabarisha, kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd: ´Abdullaah bin ´Aamir amenikhabarisha, kutoka kwa ´Aaishah, aliyesema:

“Mwanzoni wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipofika Madiynah, alikesha usiku na kusema: “Laiti mtu mwema miongoni mwa Maswahabah wangu angenilinda usiku huu.” Wakati tukiwa katika hali hiyo tukasikia mlio wa silaha, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Ni nani huyo?” Akasema: “Mimi ni Sa’d. Nimekuja kukulinda.” Baada ya hapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akalala.”[2]

114 – Muhammad bin al-Muthannaa ametukhabarisha, kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd: Ismaa´iyl ametuhadithia: Qays ametukhabarisha: Nimemsikia Sa´d bin Abiy Waqqaas akisema:

”Mimi ndiye mwarabu wa kwanza niliyerusha mshale katika njia ya Allaah.”[3]

115 – Ishaaq bin Ibraahiym ametukhabarisha: Muhammad bin ´Ubayd ametukhabarisha: Sadaqah bin al-Muthannaa ametukhabarisha, kutoka kwa babu yake Rabaah bin al-Haarith, kutoka kwa Sa´iyd bin Zayd, ambaye amesema:

“Nashuhudia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: “Abu Bakr yuko Peponi, ´Umar yuko Peponi, ´Uthmaan yuko Peponi, ´Aliy yuko Peponi, Twalhah yuko Peponi, az-Zubayr yuko Peponi, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf yuko Peponi na Sa´d yuko Peponi.” Ningetaka kutaja wa tisa, basi ningelimtaja. Mimi ndiye muumini wa tisa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ndiye muumini wa kumi.”

116 – ´Amr bin ´Aliy ametukhabarisha: Yahyaa ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa al-Miqdaam bin Shurayh, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Sa´d, ambaye amesema:

“Kuliteremshwa Aayah kwa ajili yangu na Maswahabah wengine sita wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), akiwemo Ibn Mas’uud. Wakasema: ”Ee, Mtume wa Allaah, uwafukuze watu hawa wanyonge kutoka kwako, yaani watu wako wa ndani.” Kukaingia kitu katika mawazo kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ambapo kukateremshwa Aayah isemayo:

وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ

“Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola wao asubuhi na jioni wanataka uso Wake. Si juu yako hesabu yao chochote na wala hesabu yako si juu yao chochote, hata uwafukuze, [kwani ukiwafukuza] utakuja kuwa miongoni mwa madhalimu.”[4]

[1] al-Bukhaariy (3725) na Muslim (2411).

[2] al-Bukhaariy (7231) na Muslim (2410).

[3] al-Bukhaariy (3728) na Muslim (2992).

[4] 6:52 Muslim (2413).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 84-86
  • Imechapishwa: 14/09/2026