105 – Mu´aawiyah bin Swaalih ametukhabarisha: Zakariyyaa bin ´Adiy ametukhabarisha: ´Aliy bin Mishar ametukhabarisha, kutoka kwa Hishaam bin ´Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Marwaan, ambaye amesema:
“´Uthmaan alitokwa na damu puani katika Mwaka wa Kutokwa na damu puani na akaambiwa: “Mteua atayekuja baada yako.” Akasema: ”Je, wamemtaja az-Zubayr? Akasema: “Ndiyo.” Ndipo akasema: “Naapa kwa Allaah na Yule ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake! Alikuwa ndiye mbora wao na anayependeza zaidi kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]
106 – Haajib bin Sulaymaan ametukhabarisha, kutoka kwa Wakiy´, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa Hurr bin Swayyaah, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin al-Akhnas:
“Nilikuwa na Sa’iyd bin Zayd bin ‘Amr bin Nufayl kwa al-Mughiyrah bin Shu’bah, ambaye alitaja kitu kumuhusu ‘Aliy. Ndipo akasema: ”Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Kumi katika Quraysh wako Peponi: Abu Bakr yuko Peponi, ´Umar yuko Peponi, ´Aliy yuko Peponi, ‘Uthmaan yuko. Peponi, Twalhah yuko Peponi, az-Zubeir yuko Peponi, ´Abdur-Rahmaan yuko Peponi, Sa´d yuko Peponi na Sa’iyd bin Zayd bin ´Amr.
107 – al-Qaasim bin Zakariyyaa ametukhabarisha: Abu Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa Hishaam bin ´Urwah na Sufyaan bin Sa´iyd, kutoka kwa Muhammad bin al-Munkadir, kutoka kwa Jaabir, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ni nani anayeweza kutuletea khabari kutoka kwa watu?” az-Zubayr akasema: “Mimi.” Ndipo Mtume wa Allaah Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Hakika kila Nabii anaye Swahabah na mfuasi maalum. Hakika Swahabah na mfuasi wangu maalum ni az-Zubayr.”[2]
108 – Ahmad bin Harb ametukhabarisha: Abu Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Ibn-ul-Munkadir, kutoka kwa jaabir, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”az-Zubayr ni mtoto wa shangazi yangu na Swahabah na mfuasi wangu maalum.”
109 – Muhammad bin Haatim bin Nu´aym ametukhabarisha: Hibbaan ametukhabarisha: ´Abdullaah ametukhabarisha, kutoka kwa Hishaam bin ´Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Zubayr, ambaye amesimulia:
”Siku ya Ahzaab, mimi na ´Umar bin Salamah tuliwekwa pamoja na wanawake. Nikatazama na kumuona az-Zubayr akiwa amempenda farasi wake kwenda kwa Quraydhwah mara mbili au mara tatu. Wakati aliporudi, nilimwambia: “Baba mpendwa! Nilikuona umepanda ukienda na kurudi.” Akasema: ”Umeniona kweli mwanangu?” Nikasema: “Ndio.” Akasema: “Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema: “Ni nani awezaye kwenda kwa Banu Quraydhwah na kuniletea khabari zao?” Nikaondoka. Niliporudi, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanitajia wazazi wake wote wawili na akasema: “Watolewe fidia kwako wazazi wangu!”[3]
110 – Ishaaq bin Ibraahiym ametukhabarisha: ´Abdah bin Sulaymaan ametukhabarisha: Hishaam bin ´Urwah ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Urwah, kutoka kwa ´Abdullaah bin az-Zubayr, kutoka kwa az-Zubayr, ambaye amesema:
”Siku ya Quraydhwah Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinitajia wazazi wake wote wawili na kusema: “Watolewe fidia kwako wazazi wangu!”
[1] al-Bukhaariy (3717).
[2] al-Bukhaariy (4113) na Muslim (2415).
[3] l-Bukhaariy (3720) na Muslim (2416).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 82-84
- Imechapishwa: 14/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 82-84
Imechapishwa: 14/09/2026
https://firqatunnajia.com/25-fadhilah-za-az-zubayr-bin-al-awwaam/