35- Kuoga kwa ajili ya Twawaaf.

36- Mwenye kutufu kuvaa soksi ili asikanyage uchafu kutoka chooni na vifuniko vya mikono yake ili asije kuwagusa wanawae.

37- Mwenye kuhirimia kuswali Rak´ah mbili za Tahiyyat-ul-Masjid anapoingia msikiti Mtakatifu[1].

38- Kusema: “Nimenuia kutufu wiki hii kadhaa na kadhaa.”

39- Kunyanyua mikono wakati wa kulisalimia jiwe kama kama ambavo mtu ananyanyua mikono wakati wa swalah.

40- Kupiga kura kwa ajili ya kulibusu jiwe jeusi.

41- Kuleta msongamano kwa ajili ya kulibusu na kutoa salamu kabla ya imamu ili mtu awahi kulibusu.

42- Kusimama kwenye laini kwa sababu ya kulibusu jiwe au nguzo ya yemeni.

43- Mtu kusema wakati wa kuligusa jiwe:

اللهم إيمانا بك وتصديقا بكتابك

“Ee Allaah! [Nayafanya haya] kwa kukuamini na kusadikisha Kitabu Chako.”

44- Mtu kusema wakati anapoligusa jiwe:

اللهم إني أعوذ بك من الكبر والفاقة مراتب الخزي في الدنيا والآخرة

“Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na uzee, ufukara na utwevu duniani na Aakhirah.”

45- Kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto wakati wa Twawaaf.

46- Mtu kusema mbele ya mlango wa Ka´bah:

اللهم إن البيت بيتك والحرم حرمك والأمن أمنك وهذا مقام العائد بك من النار مشيرا إلى مقام إبراهيم عليه السلام

“Ee Allaah! Hakika Nyumba ni Yako. Msikiti Mtakatifu ni Wako. Amani ni Yako. Hapa ndipo mahali pa yule aliyekuomba hifadha kutokama na Moto” na akaashiria sehemu ya kusimama pa Ibraahiym (´alayhis-Salaam).”

47- Kuomba du´aa katika nguzo ya iraki:

اللهم إني أعوذ بك من الشك والشرك والشقاق والنفاق وسوء الأخلاق وسوء المنقلب في المال والأهل والولد

“Ee Allaah! Mimi najilinda Kwako kutokamana na mashaka na shirki, vipingamizi na unafiki, tabia mbaya na mgeuko mbaya katika mali, familia na kizazi changu.”

48- Kuomba du´aa chini ya mfereji wa paa:

اللهم أظلني في ظلك يوم لا ظل إلا ظلك

“Ee Allaah! Niweke kwenye kivuli Chako siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli Chako.”

49- Mtu kuomba du´aa wakati anakwenda kwa haraka:

اللهم اجعله حجا مبرورا وذنبا مغفورا وسعيا مشكورا وتجارة لن تبور يا عزيز يا غفور

“Ee Allaah! Ijaalie kuwa ni hajj yenye kukubaliwa, dhambi yenye kughufuriwa, jitihada zenye kulipwa na biashara isiyokwenda patupu. Ee Mwenye nguvu kabisa, ee Mwenye kusamehe.”

50- Katika ile mizunguko nne yenye kubali mtu kusema:

رب اغفر وارحم وتجاوز عما تعلم إنك أنت الأعز الأكرم

“Ee Mola! Nisamehe na Unirehemu. Usamehe yale Unayoyajua. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu kabisa, mkarimu.”

51- Kuibusu nguzo ya yemeni.

52- Kuzibusu na kuzigusa nguzo mbili za Shaam na sehemu pa kusimama Ibraahiym.

53- Kugusa kuta za Ka´bah na sehemu pa kusimama Ibraahiym.

54- Kutafuta baraka kwenye kizingiti madhubuti. Ni sehemu ya juu kwenye kuta za Nyumba inayoelekea mlango wa Nyumba. Watu wasiowasomi wanadai kwamba yule atayeigusa kwa mikono yake basi atakuwa ameshikamana na kizingiti kilicho madhubuti.

55- Msumari katikati ya Nyumba. Wanaita kuwa ni “kitovu cha dunia”. Wako baadhi ya watu ambao hufunua matumbo yao na wanaweka vitovu vyao juu sehemu hiyo ili wawe wameweka vitovu vyao juu ya kitovu cha dunia.

56- Kukusudia kutufu chini ya mvua. Wanadai kwamba yule mwenye kufanya hivo basi anasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.

57- Kutafuta baraka kwa maji ya mvua yanayotiririka kutoka kwenye mfereji wa paa wenye rehema kutoka kwenye Ka´bah.

58- Kutofanya Twawaaf kwa mavazi machafu.

59- Mwenye kufanya hajj kuyamwaga maji yaliyobaki ya zamzam kwenye kisima na kusema:

اللهم إني أسألك رزقا واسعا وعلما نافعا وشفاء من كل داء

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba riziki pana, elimu yenye manufaa na dawa juu ya kila maradhi.”

60- Baadhi kuoga kwa maji ya zamzam.

61- Kuziosha ndevu kwa maji ya zamzam na kuweka pesa na nguo kwenye maji ya zamzam ili waweze kupata baraka.

62- Pindi mtu anapokunywa maji ya zamzam anapumulia ndani yake mara nyingi na anayanyanyua macho yake kila wakati na kuitazama Nyumba, kama yalivyotajwa hayo katika baadhi ya vitabu vya Fiqh.

[1] Shani ya mambo ni kwamba salamu yake ni Twawaaf kisha aswali nyuma ya mahali pa kusimama pa Ibraahiym, kama tulivyotangulia kueleza. Tazama ”al-Qawaa´id an-Nuuraaniyyah” ya Ibn Taymiyyah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 21/07/2018