25. Bid´ah za Ihraam, Talbiyah na mengineyo

23- Kuvaa viatu vyenye sifa maalum vikiwa na masharti maalum yaliyotajwa katika baadhi ya vitabu.

24- Kuhirimia kabla ya kufika katika vituo vilivyotengwa.

25- Mtu kuipitisha chini ya kwapa la kulia Ridaa´ yake kabla ya Ihraam.

26- Mtu kutamka kwa sauti nia yake.

27- Mtu kufanya hajj ya kimyakimya kwa njia ya kwamba hazungumzi.

28- Kuleta Talbiyah kwa pamoja kwa sauti moja.

29- Kusema “Allaahu Akbar” na “Laa ilaaha illa Allaah” badala ya kuleta Talbiyah.

30- Baada ya Talbiyah mtu kusema:

اللهم إني أريد الحج فيسره لي وأعني على أداء فرضه وتقبله مني اللهم إني نويت أذاء فريضتك في الحج فاجعلني من الذين استجابوا لك

“Ee Allaah! Hakika mimi nataka kuhiji. Hivyo nirahisishie. Nisaidie juu ya kutekeleza faradhi yake na Unitakabalie. Ee Allaah! Hakika mimi nimenuia kutekeleza faradhi Yako katika hajj. Hivyo nakuomba unijaalie kuwa miongoni mwa wale waliokuitikia… “

31- Kwenda kwa kuikusudia misikiti iliyoko Makkah na pembezoni mwake – tukitoa msikiti Mtakatifu. Kama mfano wa msikiti ulioko chini ya Swafaa, chini ya msikiti wa Abu Qubays, msikiti wa Mawlid na misikiti mingine ambayo imejengwa juu ya athari za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

32- Kwenda kwa kuikusudia milima na maeneo yaliyo pembezoni mwa Makkah. Kwa mfano mlima wa Hiraa´ na mlima uliyoko Minaa ambao inasemekana ndiko kulikotakiwa kuchinjwe.

33- Kwenda kwa kukusudia kuswali katika msikiti wa ´Aaishah (huko Tan´iym).

34- Kujisulubu mbele ya Nyumba[1].

[1] Inaonekana ni mtu kupangusa uso na kifua kwa mikono miwili kwa njia ya msalaba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 21/07/2018