Watu walioshikamana na dini na Sunnah wanaamini uombezi wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) uombezi kwa wapwekeshaji wahalifu na watenda madhambi makubwa, kama ilivyopokelewa katika khabari Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Abu Sa´iyd bin Hamduun ametukhabarisha: Abu Haamid ash-Sharqiy ametukhabarisha: Ahmad bin Yuusuf as-Sulamiy ametuhadithia: ´Abdur-Razzaaq ametuhadithia: Ma´mar ametukhabarisha, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Uombezi wangu ni juu ya watenda madhambi makubwa katika ummah wangu.”[1]

Abu ´Aliy Zaahir bin Ahmad ametukhabarisha: Muhammad bin al-Musayyab al-Arghayaaniy ametukhabarisha: al-Hasan bin ´Arafah ametuhadithia: ´Abdus-Salaam bin Harb al-Malaa-iy ametuhadithia, kutoka kwa Ziyaad bin Khaythamah, kutoka kwa Nu´maan bin Quraad, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa), aliyeeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nilipewa khiyari kati ya uombezi na nusu ya ummah wangu kuingia Peponi. Nikachagua uombezi, kwa sababu ni yenye kuenea na kutosheleza. Mnaona ni kwa wale waumini na wenye kumcha Allaah? Hapana. Ni kwa wale watenda madhambi, wenye kujichafua na wenye kukosea.”[2]

Abu Muhammad al-Makhladiy ametukhabarisha: Abul-´Abbaas as-Sarraaj ametukhabarisha: Qutaybah bin Sa´iyd ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Muhammad ad-Daraawardiy ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Abiy ´Amr…ح Abu Twaahir bin Khuzaymah ametukaharisha: Babu yangu, imamu, Muhammad bin Ishaaq bin Khuzaymah ametuhadithia: ´Aliy bin Hajar bin Ismaa´iyl bin Ja´far ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Abiy ´Amr, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd al-Maqburiy, kutoka kwa Abu Hurayrah, aliyesema:

”Ee Mtume wa Allaah! Ni nani katika watu atakayekuwa na furaha zaidi kwa uombezi wako?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nilikuwa na yakini ya kwamba hakuna yeyote kabla yako atakayeniuliza kuhusu swali hilo kutokana na nilivyoona pupa yako juu ya Hadiyth. Hakika atakayekuwa na furaha zaidi ya uombezi wangu siku ya Quyaamah ni atakayesema: “Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” akiwa ni wenye kutakasika kutoka moyoni mwake.”[3]

[1] Ahmad (3/213), Abu Daawuud (4739) na at-Tirmidhiy (2345).

[2] Ahmad (5452) na Ibn Maajah (4311). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwilaal-ul-Jannah” (791).

[3] al-Bukhaariy (99) na (6570).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 258-263
  • Imechapishwa: 17/12/2023