25. Ahl-us-Sunnah wanayaamini yale yote yatayotokea siku ya Qiyaamah

Watu walioshikana na dini na Sunnah wanaamini Kufufuliwa siku ya Qiyaamah na hali zote alizoeleza Allaah (Subhaanah) zitazotokea siku hiyo ya haki. Wanaamini kutofautiana kwa hali za waja na viumbe katika siku hiyo kubwa, ambazo wataziona na kukutana nazo. Madaftari yatapokelewa kwa mikono ya kuume na ya kushoto, kujibiwa kwa maswali na matetemeko ya ardhi na mabalaa mengine yatayotokea katika siku hiyo kubwa. Kutakuwepo na mambo ya kutisha katika Njia na Mizani. Yatatawanywa madaftari, ambayo yamebeba matendo mema na maovu yenye uzito sawa na mduduchungu.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 257-258
  • Imechapishwa: 17/12/2023