Swali 253: Ni ipi hukumu ya kuwatengenezea chakula wafiwa wa maiti?
Jibu: Ikiwa jamaa zake maiti wameshughulishwa na msiba kwa njia ya kwamba hawawezi kujipikia chakula chao, basi ni Sunnah kuwapikia chakula. Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofikiwa na khabari juu ya kufariki kwa Ja´far bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´ anh) akasema:
“Watengenezeeni chakula familia ya Ja´far! Hakika mambo yalivyo wamefikwa na kinachowashughulisha.”[1]
Hilo likafahamisha kuwa si jambo linalopendeza kwa njia ya moja kwa moja, hata hivyo ni jambo linalopendeza ikiwa wafiwa wa maiti wameshughulishwa kutokana na kujipikia chakula chao. Lakini ikiwa jambo ni la kawaida, kama inavyotambulika leo, hivyo itakuwa haikusuniwa kuwaagizia chakula. Kwa sababu hukumu inazunguka na sababu yake, ni mamoja kuwepo na kutokuwepo kwake. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:
“Watengenezeeni chakula familia ya Ja´far!”
hakusema kuwa ni kwa sababu wamefiwa na mtu, bali alisema:
“Hakika mambo yalivyo wamefikwa na kinachowashughulisha.”
Kutokana na hilo ikiwa hawakushughulishwa basi hawatakiwi kuagiziwa chakula. Lakini ikiwa watapata chakula na wakawa na baadhi ya jamaa, basi inafaa kwa wao kukila. Ama kuwaalika watu kuja kula ni aina fulani ya maombolezo. Kwa ajili hiyo inachukiza kwa wafiwa wa maiti kupika chakula na kuwaalika watu kula. Kwa msemo mwingine inapata kutambulika kuwa yale yanayofanywa na baadhi ya waislamu ambapo wanatengeneza chakula wakati anapofariki mtu na kuwaalika watu kuja kula ni katika Bid´ah.
[1] Ahmad (6/266), Abu Daawuud (3132) na at-Tirmidhiy (998) aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/277-278)
- Imechapishwa: 12/02/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/277-278)
Imechapishwa: 12/02/2026
https://firqatunnajia.com/253-ni-ipi-hukumu-ya-kuwatengenezea-chakula-wafiwa-wa-maiti/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket