Kitu ambacho kihakika mtu anatakiwa kulia na kuhuzunika kwa sababu yake ni pale ambapo mtu anakuwa hakuhakikisha haki za Allaah au kwa sababu mtu amechanganya matendo mema na maovu na hivyo akawa ni mwenye kuingia ndani ya utashi wa Allaah na ukiongezea juu ya hilo anakuwa na majuto makubwa kama jibali na khasara nyingi kama changarawe.
Mgonjwa tu ndiye anatambua kihakika afya njema ni kitu gani.
Aliyepewa majaribio ndiye anatambua kihakika afya ni kitu gani.
Kadhalika uhai. Hakuna anayetambua uhai ni kitu gani isipokuwa yule maiti.
Wale maiti hivi sasa wamedhihirikiwa na uhakika wa vitu na mambo. Hivi sasa wamedhihirikiwa na thamani ya matendo mema. Huko matendo mema pake yake ndio yananufaisha. Huko yule mja mwema ndiye hupandishwa hadhi. Aliyefanya upungufu atakuja kutamani lau angelirudishwa duniani ili afanye vizuri yale aliyokosa. Tamaa ya kurudi kwa yule aliyefanya vibaya ni kubwa mno. Kwa hivyo ni wajibu kutumia fursa ya kuwa na afya njema na faradha mambo ambayo watu wengi wanadanganyika navyo.
Mtu anapaswa kuhuzunika na kulia kwa yule aliyesibiwa na mambo haya kwa sababu alighafilika na uhalisia wa mauti na upweke wa ndani ya kaburi na hali yake ya utewvu na ugeni. Baada ya hapo kunakuja maswali ya Munkar na Nakiyr (´alayhimas-Salaam). Baada ya hapo kunafuata kile kipindi kirefu ambacho mtu anakuwa chini ya udongo ambapo ima mtu anakuwa katika kuneemeshwa au kuadhibiwa. Baada ya hapo kunafuata kutoka ndani ya kaburi lake na kusimama mbele ya Mola wa walimwengu. Baada ya hapo kunafuata kusimama kwa muda mrefu kwenye uwanja wa mkusanyiko na hali mbalimbali zitazoonekana huko siku ya Qiyaamah. Baada ya hapo kuna hesabu atayofanyiwa mbele ya Allaah (Ta´ala) na matendo yake kupimwa. Kuna madaftari ya hesabu ambayo yatakuwa na uzito sawa na punje ndogo ya mbegu. Atapata kila alichokifanya kimerekodiwa kwenye kitabu kisichoacha dogo wala kubwa ila imekidhibiti. Mtu atakuwa baina ya matarajio na khofu. Ataenda ima katika kundi la upande wa kulia au upande wa kushoto.
Endapo yule msibiwaji atazingatia misiba hii mikubwa inayomsubiri na ambayo ameghafilika nayo na ambayo hakujiandaa nayo, yatamfanya kusahau misiba ya wapenzi wake na kurudi katika subira na kuridhia yale Allaah aliyokadiria na kukiacha kipite. Ikiwa anaweza kunufaisha kwa kitu, anaweza kumnufaisha maiti wake kwa hilo. Ikiwa hawezi kufanya hivo basi angalau asimuudhi yule maiti kwa yale ambayo Shari´ah imekataza kujiadhibu, kupiga mayowe, kupiga mashavu, kuchana nguo na matendo na maneno mengine yaliyokemewa na Salaf.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 44-45
- Imechapishwa: 14/10/2016

Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 44-45
Imechapishwa: 14/10/2016
https://firqatunnajia.com/25-maiti-tu-ndiye-hutambua-thamani-ya-uhai/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)