Yule mwenye kusibiwa anapaswa kujua pia kwamba kulia kunamdhuru aliye hai na yule maiti. Mliaji kuna khatari akapoteza kuona. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Ya´quub (´alayhis-Salaam):

وَابْيَضَّتْ عَيْنَاهُ مِنَ الْحُزْنِ فَهُوَ كَظِيمٌ

“Macho yake yakageuka meupe [kwa kulia] kutokana na huzuni.” (12:84)

Kadhalika hastarehi kwa kule kulia. Abu Shujaa´ ad-Daylamiy amepokea kwa mlolongo wa wapokezi wake kutoka kwa ´Aliy bin al-Husayn ambaye amesema:

“Wakati ambapo Daawuud at-Twaa´if alikuwa amekaa pamoja na marafiki zake alipitikiwa na usingizi mara moja halafu akaamka haraka na kusema: “Mnajua nilichoota?” Nimeota kuwa nimeingia Peponi na kuona watoto wanacheza na tufah walilokuwa wakirushiana. Pembezoni kulikuwa na mtoto ambaye alikuwa anaonekana kuwa ni mwenye kusikitika na mwenye huzuni. Nikauliza: “Kwa nini mtotot yule hachezi na wenzake?” Wakasema: “Amekufa hivi karibuni na mama yake analia sana kwa sababu yake. Anahuzunika kwa sababu mama yake anamlilia.” Nikauliza: “Wanakaa wapi?” Wakasema: “Katika kabila kadhaa.” Nikauliza: “Wazazi wake ni kina nani?” Wakasema: “Fulani na fulani.” Nikauliza: “Yeye anaitwa nani?” Wakasema: “Fulani.” Daawuud akasema kuwaambia marafiki zake: “Hebu twende.” Wakaenda na kufika katika kabila hilo na wakawaulizia wazazi. Wakakutana nao au mmoja wao. Akawaeleza alichokiota. Ndipo mama akaapa laiti asingelia kwa ajili yake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 44
  • Imechapishwa: 14/10/2016