125 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Daawuud bin al-Muhabbar ametuhadithia: A´yun Abul-Ahwas ametuhadithia: Nimemsikia Maalik bin Diynaar akisema:

”Haitakikani kwa mwenye busara kumilikiwa na matamanio yake ya chakula na mavazi.”

Amesema tena:

”Wakati mmoja nilikula chakula na nikahisi kiburi.”

Nimemsikia akisema:

”Njaa inafukuza kiburi na shibe inazalisha na kuikuza.”

126 – Muhammad amesema: Zayd bin al-Habbaab ametuhadithia: Muhammad bin Hawshab ametuhadithia: Nimemsikia Muhammad bin Waasiy´ akisema:

”Chumo zuri linatakasa miili. Allaah amrehemu anayekula kizuri na akalisha kizuri.”

127 – Muhammad amesema: ´Ubaydullaah bin Muhammad amenihadithia: Muhammad bin al-Ja´d amenihadithia, kutoka kwa Ziyaad an-Numayriy, amesema:

”Tumefikiwa na khabari mtu ataitwa siku ya Qiyaamah, ambapo atasimama kati ya safu zote. Nuru yake itazidi mpaka aambiwe: ”Ni nani huyu ambaye nuru yake imeongezeka?” Aite kwa sauti mwitaji: ”Huyu ni mtu ambaye alipatwa na njaa na kuwa na kiu kwa ajili ya Allaah duniani.”

128 – Muhammad amesema: ´Ubaydullaah bin Muhammad ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Ayyaash ametuhadithia, kutoka kwa baadhi ya wanamme wake, ambaye amesema:

”Imeadikwa katika vile vitabu vya kale: ”Pepo kwa yule ambaye amepatwa na njaa kwa ajili ya ile siku ya Shibe kubwa! ”Pepo kwa yule ambaye amepatwa na kiu kwa ajili ya ile siku kubwa ya umwagiliaji!”

129 – Muhammad ametuhadithia: ´Ubaydullaah ametuhadithia: Salamah bin Sa´iyd ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Shaabuur, ambaye amesema:

”Tumefikiwa na khabari kwamba wale watakaohutubia watu wa Peponi siku ya Qiyaamah baada ya Mitume ni wale wenye njaa na wenye kiu.”

130 – Muhammad bin Idriys amenihadithia: Ahmad bin Abiyl-Hawaariy ametuhadithia: Muhammad bin Mu´aawiyah Abu ´Abdillaah as-Suuriy ametuhadithia: Nimemsikia baba yangu akisema:

”Mja hali akashiba isipokuwa huondokewa na sehemu ya busara isiyomrejelea katu.”

131 – Muhammad bin Idriys amenihadithia: Ahmad bin Abiyl-Hawaariy ametuhadithia, kutoka kwa Muusa bin Daawuud: Nimemsikia ´Abdullaah bin Marzuuq akisema:

”Yule anayekusanya kati ya mafuta na sukari huyapuuza madhambi yake.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 89-91
  • Imechapishwa: 23/07/2023